Wednesday, 1 July 2015

hukuona video ya shilole alivyomvalisha nuhu mziwanda pete? ni muda wako kuona vituko vyao na mate nje nje

Ghana yazindua gari lake. ni hatua kubwa kufanyika barani afrika, lione hapa




Gari la kantanka nchini Ghana

Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko.
Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.


null
Gari aina ya kantanka

Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.


null
Magari aina ya kantanka

Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya magharibi ni


null
Gari aina ya kantanka

bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari langu rasmi.


null
Magari aina ya kantanka kutoka Ghana

Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.


null
Gari aina ya kantanka

Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini Ghana litapata umaarufu.

Mashambulio mabaya yatokea Misri angalia hapa



Rasi ya Sinai
Rasi ya Sinali imeshuhudia mashambulizi ya kila mara
Makundi ya wapiganaji yamefanya misururu ya mashambulio dhidi ya maafisa wa usalama nchini Misri katika Rasi ya Sinai.
Jeshi limesema makabiliano yanaendelea huku wanajeshi kadhaa na wapiganaji wakiuawa.Taarifa ya jeshi imesema vizuizi vitano vya polisi vililengwa sawa na kituo kimoja cha polisi.
null
Wapiganaji wa Kiisilamu wamekuwa wakiwalenga wanajeshi
Hili ndilo shambulio kubwa zaidi kufanywa na wapiganaji wa kiisilamu walioko eneo la Sinai, miaka miwili baada ya kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeegemea mrengo wa kidini Mohamed Morsi.
Tukio hili limejiri siku moja baada ya Rais wa Misri Abdul Fattah al Sisi kuapa kupendekeza sheria mpya za kukabiliana na ugaidi. Hapo Jumatatu mwendesha mashtaka wa Misri aliuawa katika shambulio la bomu iliyotegwa ndani ya gari.

behind the scene au nyuma ya kamera ya wimbo wa mdogo mdogo hii hapa kama haukubahatika kuiangalia

WADADA KUA UCHI KATIKA HII VIDEO YA MUSTAFA COLONEL WA KENYA WAIFANYA IZUILIWE KUCHEZWA KATIKA TV ZA KENYA

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...