Thursday, 19 June 2014

RAISI MSHTAKIWA WA SIERRA LEONE CHARLES TAYLOR APINGA KUTUMIKIA KIFUNGO UINGEREZA

Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za
kisheria kupinga amri ya kutumikia kifungo chake cha jela
nchini Uingereza.
Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu na anakataa
kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa
haki ya kufurahia maisha yake.
Charles Tayor anatumikia kifungo cha miaka hamsini jela kwa
makosa ya ubakaji na kutumia watoto kama wanajeshi wakati
wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.
Mawakili wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake nchini
Uingereza kunakiuka haki za binadamu kwa sababu ni mbali
sana na yumbani kwa familia yake kuweza kusafiri huko
kumuona.
Wanasema kuwa badala ya kutumikia kifungo Uingereza,
aruhusiwe kutumikia kifungo hicho nchini Rwanda, pamoja na
wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama maalum ya
umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.
Pia wanasema anahofia kushambuliwa na wafungwa wengine
katika gereza la Frankland, Kaskazini mwa Uingereza.

MAREKANI SASA YAIWEKEA UGANDA VIKWAZO VIKALI BAADA YA KUPINGA SERA YA USHOGA

Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika
ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua
kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la
Uganda mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.
Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati
waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na
ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.
Sekta ya Afya na usalama wa taifa itaathirika na vikwazo hivyo.
Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa
marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa
mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya
Marekani.
Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia
moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo
cha maisha jela.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani
katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.
Juma lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten
Gillibrand alilalmikia vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya
kigeni wa Uganda Sam Kutesa kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja
wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea Uganda.
Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya
wapenzi wa jinsia moja.
Watu 9000 walikuwa wametia sahihi pendekezo la kuitaka
Umoja wa Mataifa kumng'oa kitini bw Kutesa aliyechaguliwa
licha ya kampeini hiyo.
Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda
mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa
kupingwa kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi
kudhihirishia wafuasi wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo
kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya benki kuu ya
dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo
zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini
Uganda .
Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na
Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika
Mashariki.

WYNE ROONEY AFUNGA NA KUSHEREKEA GOAL LA KWANZA KUIFUNGIA TIMU YAKE KATIKA KOMBE LA DUNIA LICHA YA TIMU HIYO YA UINGEREZA KUWA KATIKA HATARI YA KUONDOLEWA KATIKA MICHUANO HIYO

Mbio za kuwania ubingwa wa dunia zinazidi kushika,
na hivi punde umemalizika mchezo kabambe
uliowakutanisha Uruguay dhidi ya England.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 2-1 wa
Uruguay.
Luis Suarez akitoka kwenye majeruhi ya goti
ameiwezesha timu kupata ushindi muhimu mbele
ya England.
Suarez alianza kuifungua Uruguay kabla ya Rooney
hajasawazisha, likiwa ndio goli lake la kwanza katika
fainali 3 za kombe la dunia.
England wakiwa na kasi ya kutafuta goli la ushindi,
Suarez tena akawashangaza kwa kufunga goli la pili
kwa mkwaju mkali na mpaka refa anamaliza mpira
Uruguay walikuwa kifua mbele.
Matokeo hayo yanamaanisha England wanakaribia
kuondolewa kwenye mashindano haya, baada ya
kufungwa mechi ya pili., wakipoteza mechi yao
kwanza dhidi ya Italy.
Mpaka sasa timu kubwa za Spain, Australia na
Cameroon zimeshaaga mashindano hayo.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...