Thursday, 19 June 2014

RAISI MSHTAKIWA WA SIERRA LEONE CHARLES TAYLOR APINGA KUTUMIKIA KIFUNGO UINGEREZA

Rais wa zamani wa Liberia, ameanzisha harakati za
kisheria kupinga amri ya kutumikia kifungo chake cha jela
nchini Uingereza.
Taylor alifungwa jela kwa uhalifu dhidi ya binadamu na anakataa
kutumikia kifungo hicho Uingereza akisema kuwa ananyimwa
haki ya kufurahia maisha yake.
Charles Tayor anatumikia kifungo cha miaka hamsini jela kwa
makosa ya ubakaji na kutumia watoto kama wanajeshi wakati
wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone.
Mawakili wake wanasema kuwa kuzuiliwa kwake nchini
Uingereza kunakiuka haki za binadamu kwa sababu ni mbali
sana na yumbani kwa familia yake kuweza kusafiri huko
kumuona.
Wanasema kuwa badala ya kutumikia kifungo Uingereza,
aruhusiwe kutumikia kifungo hicho nchini Rwanda, pamoja na
wafungwa wengine waliohukumiwa na mahakama maalum ya
umoja wa mataifa kuhusu Sierra Leone.
Pia wanasema anahofia kushambuliwa na wafungwa wengine
katika gereza la Frankland, Kaskazini mwa Uingereza.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...