Thursday, 19 June 2014

MAREKANI SASA YAIWEKEA UGANDA VIKWAZO VIKALI BAADA YA KUPINGA SERA YA USHOGA

Afisa wa mahusiano anayesimamia maswala ya usalama katika
ikulu ya whitehouse Caitlin Hayden anasema kupitia kwa barua
kwa wanahabari kuwa sheria hiyo iliyopitishwa na bunge la
Uganda mwezi Februari inakiuka haki za binadamu.
Vikwazo hivyo vitajumuishwa marufuku ya wanaharakati
waliopigia debe sheria hiyo kupitishwa kutoingia Marekani.
Miradi itakayoathirika na marufuku hiyo ni pamoja na
ushirikiano na polisi wa Uganda Wizara ya Afya.
Sekta ya Afya na usalama wa taifa itaathirika na vikwazo hivyo.
Aidha msaada kwa miradi iliyoanzishwa kwa usaidizi wa
marekani pia utapunguzwa mbali na kufutiliwa mbali kwa
mazoezi ya kijeshi kati ya majeshi ya uganda na yale ya
Marekani.
Sheria hiyo inaharamisha uhusiano baina ya watu wa jinsia
moja na wale watakaopatikana wanaweza kuhukumiwa kifungo
cha maisha jela.
Hii ndiyo hatua ya hivi karibuni iliyochukuliwa na Marekani
katika ajenda yake ya kupinga sheria hiyo mpya nchini Uganda.
Juma lililopita Seneta mmoja kutoka Marekani ,Kirsten
Gillibrand alilalmikia vikali uteuzi wa waziri wa maswala ya
kigeni wa Uganda Sam Kutesa kuchaguliwa kuwa rais wa Umoja
wa Mataifa kutokana na kuwa anatokea Uganda.
Marekani imeiwekea Uganda vikwanzo kuhusina na sheria ya
wapenzi wa jinsia moja.
Watu 9000 walikuwa wametia sahihi pendekezo la kuitaka
Umoja wa Mataifa kumng'oa kitini bw Kutesa aliyechaguliwa
licha ya kampeini hiyo.
Wanaharakati wa wapenzi wa jinsia moja wameenda
mahakamani wakitaka sheria hiyo iondolewe lakini inatarajiwa
kupingwa kwani rais Yoweri Museveni aliupitisha maksudi
kudhihirishia wafuasi wake kuwa yu huru kutokana na shinikizo
kutoka kwa mataifa ya ughaibuni .
Punde baada ya kupitishia kwa sheria hiyo mpya benki kuu ya
dunia iliahirisha utoaji wa mkopo wa dola milioni 90 ambazo
zilikuwa zinapaswa kutumika kuimarisha sekta ya Afya nchini
Uganda .
Mataifa mengi tu ikiwemo Denmark, Norway, Uholanzi na
Sweden zote zimekatiza msaada kwa taifa hilo la Afrika
Mashariki.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...