Wednesday, 11 May 2016

Video: mtazame huyu mwanafunzi mrefu ajabu kuwahi tokea barani afrika.

Maajabu:Mtazame mwanafunzi huyu mwenye jinsia ya kike na kiume.

Mwanamke aunda boti lenye umbo la uke wake


Image copyrightAFP
Image captionBoti iliofanana na uke
Mahakama moja ya Japan imempata msanii mmoja bila hatia ya kutengeza boti iliyofanana na uke wake.
Jaji aliamuru kwamba boti ya Megumi Igarashi iliofanana na uke wake na yenye rangi nyingi haikuashiria umbo la uke.
Hatahivyo ,alipigwa faini ya dola 3,700 baada ya jaji kuamuru hakuvunja sheria kwa kusambaza data ya uke wake ambayo inaweza kutumika kutengeza umbo la uke wake.
Sheria kali za Japan zinapinga kuonyeshwa hadharini kwa sehemu za siri.
Igarashi mwenye umri wa miaka 42,kwa jina Rokudenashiko au ''good for nothing girl'' alikamatwa mwaka 2014 baada ya boti yake kuonyeshwa katika duka moja la vifaa vya ngono mjini Tokyo.
Image copyrightAFP
Image captionMegumi Igarashi
Alishtakiwa chini ya sheria ya mambo machafu kwa kuonyesha boti hiyo na kusambaza data yake kwa wale waliochangisha fedha ili itengezwe.
Siku ya Jumatatu jaji mmoja aliamua kwamba rangi zake zinazong'aa na mapambo yake hayaonyeshi ukweli wa umbo la uke.
''Lakini data yake licha ya kutokuwa na umbo la uke itatumika kutengeza uke wa Bi Igarashi kwa kutumia 3D na hivyobasi ni uchafu'',alisema jaji.
Bi Igarashi alipigwa faini nusu ya Yen 800,000 zilizohitajika na afisi ya mashtaka.

huzuni:watu 50 wafariki kwenye mafuriko Ethiopia.tazamani



Image copyrightUGC
Image captionMaeneo mengi ya Afrika mashariki yameathirika na mafuriko
Takriban watu 50 wamefariki kufautia mafuriko na maporomoko ya ardhi yaliosababishwa na mvua kubwa katika baadhi ya maeneo Ethiopia.
Taifa hilo la upembe wa Afrika linakabiliwana ukame mbaya kuwahi kushuhudiwa katika miaka 50 huku watu zaidi ya milioni 10 wakiwa wanahitaji msaada wa dharura wa kibinaadamu.
Ukame huo umezidhishwa kuwa mbaya kutokana mvua ya El Nino inayoaathiri baadhi ya mataifa Afrika mashariki na kusini.
Maafisa wa serikali katika wilaya iliopo kusini mwa Ethiopia Wolaita wamekiambia kituo cha televisheni ya serikali kuwa watu 41 waliuawa Jumatatu katika maporomoko ya ardhi yaliotokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini.
Wengine 9 walifariki kuisni mashriki mwa eneo la Bol ambako mamia ya mifugo pia ilizama.
Maelfu ya watu pia wamepoteza makaazi yao, walisema maafisa.
Mafuriko yametatiza jitihada za kuwaisaidia watu wanaohitaji usaidizi baada ya barabara nyingi na vivukio kuharibika kabisa.
Serikali na mashirika yamisaada yameanzisha ombi la msaada wa thamani ya dola bilioni 1.4 kuwasiaidia mamilioni ya watu wanaohitaji kwa dharura chakula.

mwanasiasa Besigye atiwa mbaroni vikali kwa 'kujiapisha' Uganda


Image copyrightAP
Image captionBesigye akamatwa kwa 'kujiapisha' Uganda
Taharuki imetanda nchini Uganda baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais Yoweri Museveni .
Haijulikani ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi cha polisi na kuibukia mjini Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha urais wa taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo imesambazwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii.
Image captionRais Yoweri Museveni kuapishwa Alhamisi
Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya kuwa ''endapo kutafanyika sherehe nyengine hapo kesho, basi itakuwa ni kinyume cha sheria kwani kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi wowote''.
Mgombea huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Forum for democratic change FDC- alikamatwa na polisi kwa'' kukaidi amri halali''.
Matukio hayo yanawadia wakati ambao viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na wageni mashuhuri wameanza kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria kuapishwa kwa rais Museveni hapo kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi kutangazwa mwezi Februari, Dr Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi mkali nyumbani kwake baada ya kupinga matokeo yaliyompa rais Museveni ushindi.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...