![]() |
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones |
Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAMPARD imeitupa nje ya mashindano ya kombe la ligi MANCHESTER UNITED baada ya kuitandika kwa penati 8-7 kufuatia sare ya mabao MAWILI kwa MAWILI kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la OLD TRAFFORD.
Katika mchezo huo HARRY WILSON amekuwa mchezaji wa kwanza kuifunga MANCHESTER UNITED goli la moja kwa moja la mpira wa adhabu yaani Direct Free Kick katika kombe la ligi kwenye dimba la OLD TRAFFORD tangu alipofanya hivyo GILES BARNES mwezi JANUARY mwaka 2009 wakati akifunga bao la kwanza la kusawazisha kwa DERBY COUNTRY.
MANCHESTER UNITED imepoteza mechi zake TANO zilizopita katika mashindano yeto ambazo ziliamuliwa na changamoto ya mikwaju ya penati ambapo TATU ni za kombe la ligi, moja kwenye kombe la FA na nyingine kwenye ngao ya jamii.
![]() |
Derby wamepata ushindi wa kwanza kwenye dimba la Old Trafford tangu mwaka 2001 |
Mlinda mlango SERGIO ROMERO ni mchezaji wa kwanza wa MANCHESTER UNITED kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye dimba la OLD TRAFFORD katika mashindano yote tangu alipofanya hivyo mlinzi ERIC BAILLY mwezi MAY mwaka jana 2017 katika mchezo wa ligi ya YUROPA dhidi ya CELTA VIGO baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 67.
![]() |
Wachezaji wa Derby wakishangilia moja ya goli walilowafunga Man Utd |
Baadhi ya matokeo mengine ya michezo ya kombe la ligi MAN CITY wakiwa ugenini wameilaza OXFORD UNITED mabao MATATU kwa BILA, WEST BROM wamenyukwa mabao MATATU kwa BILA pia na CRYSTAL PALACE wakati BOURNAMOUTH wakiinyuka BLACKBURN ROOVERS mabao MATATU kwa MAWILI huku BURTON ALBION wakiishangaza BURNLEY kwa kuitandika mabao MAWILI kwa MOJA.
Hii leo kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka ambapo majogoo wa jiji LIVERPOOL watakuwa nyumbani kuwakaribisha CHELSEA wakati ARSENAL wakiumana na BRENTFORD huku TOTTENHAM HOTSPURS wakiwakaribisha WATFORD.
No comments:
Post a Comment