![]() |
Nahodha wa African Lyon Haruna Moshi amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu |
Nahodha wa AFRICAN LYON, HARUNA MOSHI maarufu kama BOBAN amesema licha ya kupoteza mchezo dhidi ya MTIBWA SUGAR bado wanaimani kikosi chao kipo kwenye kiwango kizuri kitakachowawezesha kumaliza ligi katika nafasi za juu.
MOSHI anasema timu yao ina mchanganyiko wa wachezaji vijana na wakongwe wenye uwezo wa kupata matokeo wakati wowote hivyo mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa kwani wao kama wachezaji wapo tayari kupambana mpaka tone la mwisho .
Mpaka sasa AFRICA LYON imeshacheza michezo SITA ya ligi kuu msimu huuu ambapo imeshinda mchezo MMOJA na kupoteza michezo MITATU huku ikitoka sare katika michezo MIWILI.
No comments:
Post a Comment