![]() |
Chris Smalling |
Mlinzi wa kati Manchester United Chris Smalling anataka kusaini mkataba mpya huko Old Trafford. Mchezaji huyo wa kimataifa wa ENGLAND mwenye miaka 28 amebakiza chini ya miezi 12 kwenye mkataba wake wa sasa. (Star)
Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Mjerumani Mario Gotze, 26, ameshuriwa kujiunga na meneja wake wa zamaniaJurgen Klopp huko Liverpool. (Sky Sports)
![]() |
Mrio Gotze Kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund |
David Beckham anafanya mazungumzo na mchezaji mwenzake wa zamani wakiwa Real Madrid Zinedine Zidane kuhusu kukisimamia klabu yake ya Inter Miami katika ligi ya MLS. (Mirror)
![]() |
Beckham na Zidane enzi wakicheza pamoja Real Madrid |
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema anahisi kuwa katika hali nzuri asilimia 200 licha ya kupumzishwa na meneja Maurizio Sarri kati kati ya wiki. Alirudi uwanjani akiwa kikosi cha kwanza wakati wa mechi iliyomalizika kwa sare siku ya Jumapili na West Ham. (Sky Sports)
![]() |
Eden Hazard amekuwa kwenye kiwango murua sana msimu huu |
Kipa mwenye miaka 25 wa Besiktas Loris Karius -ambaye yuko kwa mkopo huko Liverpool anasema anapata motisha kutoka kwa kipa wa zamani wa Ujerumani Olivier Kahn. (Bild - in German)
#BBC
No comments:
Post a Comment