![]() |
Luca Modric ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa FIFA katika hafla ilifanyika kwenye ukumbi wa Royal Festival mjini London |
Kiungo wa kimataifa wa CROATIA, LUCA MODRIC ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa FIFA baada ya kuwashinda CRISTIANO RONALDO na MOHAMED SALAH.
Nyota huyo anayechezea REAL MADRID aliisaidia klabu hiyo kushinda mataji MATATU mfululizo ya ligi ya mabingwa barani ulaya pamoja na kulisaidia taifa lake la CROATIA kufika fainali ya kombe la FIFA la dunia.
![]() |
Ronaldo na Messi wameshinda tuzo zote kubwa tangu mwaka 2008 |
Hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 10 kupita tuzo kubwa duniani kunyakuliwa na mchezaji tofauti ya RONALDO na MESSI ambapo mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2007 pale mbrazil RICARDO KAKA lisposhinda tuzo ya Balon d’or.
Kwa upande wa goli bora la mwaka tuzo imeenda kwa MOHAMED SALAH wa LIVERPOOL ambapo bao lake alilofunga dhidi ya EVERTON mwezi DESEMBA mwaka jana limeteuliwa kuwa goli bora la mwaka.
![]() |
Salah akifunga goli lililoshinda tuzo ya goli bora la FIFA dhidi ya Everton mwezi Desemba mwaka jana |
Ushindi huo hata hivyo umeibua mjadala hasa kutokana na ubora wa magoli mawili yaliyoshindwa likiwemo goli la CRISTIANO RONALDO dhidi ya JUVENTUS na lile la GARETH BALE dhidi ya LIVERPOOL katika michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Tuzo ya kocha bora wa mwaka imeenda kwa DIDIER DESCHAMP wa UFARANSA aliyewashinda ZINEDINE ZIDANE na ZLADKO DALIC wa CROATIA.
![]() |
Kocha wa zamani wa Arsena Arsene Wenger akimkabidhi tuzo ya kocha bora Didier Deschamp |
Tuzo ya mchezaji bora wa kike ikienda wa MARTA wa BRAZIL ambaye ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya SITA mfululizo.
![]() |
Marta mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa kike |
Tuzo ya mashabiki bora ikienda kwa mashabiki wa timu ya taifa ya PERU. Zaidi ya mashabiki arobaini elfu wa Peru walisafiri hadi Russia kuishuhudia timu yao ya taifa ikicheza fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 36.
![]() |
Mashabiki wa Peru wakiishangilia timu yao huko Russia |
No comments:
Post a Comment