Monday, 24 September 2018

Ronaldo azidi kutunisha akaunti ya mabao Italia

Ronaldo akishangilia baada ya kufunga bao dakika 9 kabla ya mchezo kumalizika
Cristiano Ronaldo ameendelea kudhihirisha kuwa yeye ni mfumania nyavu bora baada ya kuifungia JUVENTUS bao la kwanza katika ushindi wa mabao MAWILI kwa BILA dhidi ya Frosinone katika dakika ya 81.
Goli la alilofunga Ronaldo ni la TATU kwa msimu huu baada ya juma lililopita kufunga mabao mawili na mashabiki wengi wa JUVENTUS wanaamini mchezaji huyo aliyesajiliwa akitokea REAL MADRID sasa amerejea kwenye makali yake ya upachikaji mabao
Ushindi huo unawafanya JUVE kuwa na muendelezo wa ushindi kwa asalimia 100 kwenye ligi ya SERIE A kwa msimu huu baada ya kushinda michezo yao yote 5 ya mwanzo wa msimu na kufikisha alama 15 wakiwa kileleni.

Baadhi ya matokeo michezo ya serie a  iliyochezwa jana 23 SEPTEMBER 2018

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...