Friday, 22 April 2016

Kenyatta atoa dola 10m za kusaidia kilimo cha mirungi,wakati tanzania tukiipiga vita zao hilo.


Image copyright BBC World Service
Image caption Mirungi imepigwa marufuku katika baadhi ya nchi Ulaya
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba serikali yake itatenga dola za Kimarekani 10 milioni za kusaidia wakulima wa mirungi kwenye bajeti ya mwaka ujao wa kifedha.
Wakulima hao wameathirika sana kufuatia hatua ya baadhi ya nchi za Ulaya kupiga marufuku uuzaji wa mirungi, maarufu pia kama miraa, katika mataifa hayo.
Hutumiwa sana na watu wa jamii ya Wasomali na hutegemewa sana na jamii zianzoishi katika maeneo ya mashariki ya Mlima Kenya, miongoni mwa watu wa jamii ya Wameru.
Pesa hizo zitatolewa kupitia Wizara ya Kilimo.
Rais Kenyatta ametangaza hayo alipokuwa akitia saini mswada unaotambua mirungi kuwa mmea wa kuzalishia taifa mapato kuwa sheria.
Sheria hiyo itaifanya serikali kuweka mikakati ya kutangaza, kuzalisha na kusambaza na kuuza zao hilo.
Rais Kenyatta amesema kutaundwa pia jopo kazi la kuangazia changamoto zinazokabili sekta ya ukuzaji wa mirungi ambayo itatoa mapendekezo kwa serikali.

huyu ndiye mwanamuziki tajiri wa kike uingereza,mjue hapa.




Image caption Adele

Adele ametangazwa kuwa mwanamuziki tajiri wa kike nchini Uingereza,kulingana na gazeti la Sunday Times.
Orodha ya wanamuziki 50 mamilionea nchini Uingereza na Ireland inaonyesha utajiri wa mwanamuziki huyo kuwa pauni milioni 85 katika nafasi ya 30 ikiwa amejiongezea pauni milioni 35 ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Mwanamuziki pekee wa kike mwenye utajiri katika orodha hiyo inayoorodhesha taifa la Ireland ni mwanamke wa Ireland Enya mwenye utajiri wa pauni miloni 91.
Kwa mwaka wa tano mfululizo Adele ameorodheshwa katika kilele cha wanamuziki vijana wasio zidi umri wa miaka 30.


Image copyright Getty Images
Image caption Adele akitumbuiza
Utajiri wa mwanamuziki huyo uliongezeka kufuatia kutolewa kwa albamu ya 25,ikiwa ni yake ya kwanza baada ya miaka minne.
Mwanamuziki huyo aliorodheshwa wa 9 mwaka 2011,lakini ilipofikia mwaka 2012 alikuwa kileleni hadi kufikia sasa.

uingereza yawatahadharisha wapenzi wa jinsia moja.


Image copyright GETTY IMAGES
Image caption Harusi ya wapenzi wa jinsia moja Uingereza
Serikali ya Uingereza imewaonya wapenzi wa jinsia moja wanaosafiri kuelekea Marekani kutokana na sheria dhidi yao katika majimbo ya North Carolina and Mississippi.
Marekani ni jamii kubwa ilio na maoni tofauti.Sheria mpya zilizopitishwa katika majimbo hayo zinaruhusu wafanyibiashara kuamua iwapo wanaweza kuwahudumia watu wa jinsia hiyo au la.
Ushauri huo umetoka katika afisi ya maswala ya kigeni ya Uingereza.
Katika jimbo la Carolina,sheria iliopitishwa na Gavana Pat McCrory inasema kuwa watu waliobadili jinsia watumie msaala wa kuogea kulingana na jinsia yao iliopo katika vyeti vyao vya kuzaliwa.
Sheria ya Mississippi pia ina sheria kama hiyo na inawalinda wafanyibiashara wengi kytoshtakiwa kwa kukataa kuwauzia wapenzi wa jinsia moja.

mcheza filamu za ngono (x) na miereka afariki,tazama picha zake na habari hapa.



Image caption Mcheza miereka na nyota wa filamu za ngono Chyna afariki

Aliyekuwa mchezaji miereka na nyota wa filamu za ngono Chyna amefariki akiwa na umri wa miaka 45.
Meneja wake amethibitisha habari hiyo kupitia mtandao wake wa Twitter.
''Ni masikitiko makubwa kutangaza kwamba tumempoteza shujaa'',ulisema ujumbe huo,akiongezea kuwa:Ataishi kukumbukwa na mashabiki wake wengi na sisi sote tuliompenda.
Chyna alipatikana amefariki nyumbani kwake katika ufukwe wa bahari wa Redondo,mjini California,baada ya kurudi nyumbani kutoka Japan.


Image caption Chyna alipochumbiwa na mchezaji mwenza wa miereka
Mapema wiki hii alichapisha kanda ya video yenye urefu wa dakika 13 ambapo anazungumza kuhusu kuanzisha biashara mpya ya chakula.
Alionekana akikosea baadhi ya maneno aliyokuwa akiyatamka na anaonekana amechanganyikiwa.
Alijitahidi kukabiliana na dawa za kulevya wakati wote wa kazi yake na alionekana katika kituo cha kuwarekebisha tabia watu maarufu mwaka 2008.

maajabu:Marehemu ateuliwa kusimamia mechi Nigeria,soma hii


Image caption Shirikisho la Soka la Nigeria linakabiliwa na mzozo wa uongozi
Mwanamume aliyefariki ameteuliwa kusimamia mechi ya soka nchini Nigeria ambayo itachezwa Jumapili, mwandishi wa BBC anayefuatilia masuala ya soka Oluwashina Okeleji anasema.
Wale Akinsanya aliteuliwa kuwa mwamuzi kwenye mechi baina ya Warri Wolves na Giwa FC katika mji wa Warri kusini mwa Nigeria, gazeti la Punch la Nigeria limeripoti.
Hii ni licha ya kwamba Akinsanya alifariki tarehe 22 Januari 2016 wakati wa kufanywa kwa mtihani wa Fifa Cooper Test, ambao hutumiwa kuamua iwapo marefarii wanatosha kuendelea kusimamia mechi.
Aliteuliwa kusimamia mechi hiyo na mrengo wa Shirikisho la Soka la Nigeria (NFF) unaoongozwa na
Chris Giwa.

maajabu:Msomi avua nguo kwa kufungiwa ofisi,mtazame hapa

Image caption Stella Nyanzi alikuwa akimuunga mkono mgombea urais Kizza Besigye
Hatua ya mwanamke mmoja msomi ya kuvua nguo nchini Uganda imezua mjadala mkali nchini humo.
Baada ya kukerwa na hatua ya kufungiwa nje ya ofisi yake na usimamizi wa chuo kikuu cha Makerere, Stella Nyanzi alivua nguo zote kama njia ya kupinga.
Hata hivyo mwishowe aliruhusiwa kuingia ofisini mwake. Wengi wa wafuasi wake wanasema kuwa alilazimishwa kufanya hivyo kutoka na yake alikuwa akitendewa.
Hata hivyo wale wanaomkosoa wanasema kwa amekiuka maadili na kwamba mwanamke hastahili kuwa uchi hadharani.
Gazeti la the New Vision nchini humo linasema kuwa waziri anayehusika na maadili anataka Nyanzi akamatwe.

tazama: Australia jino kubwa la nyangumi lapatikana.tazama picha za nyangumi na jino hapa.


Image copyright AFPMuseum Victoria
Image caption Jino hilo lilipatikana mwezi Februari
Jino kubwa la nyangumi limepatikana ufukweni Australia, na kuwa thibitisho la kwanza kwamba nyangumi wakubwa hatari sana waliishi mbali na Amerika.
Mkusanyaji wa visukuku Murray Orr alipata jino hilo lenye urefu wa sentimeta 30 (inchi 12) ufukweni Beaumaris Bay karibu na mji wa Melbourne mwezi Februari.
Alilikabidhi kwa makumbusho ya Victoria, ambayo yalianza kulionesha kwa umma Alhamisi.
Inakadiriwa kwamba nyangumi mwenye jino hilo aliishi zaidi ya miaka milioni tano iliyopita. Alitoka kwa aina ya nyangumi ambao siku hizi hawapatikani duniani.
Nyangumi hao wanaaminika kuwa watangulizi wa nyangumi wakubwa wa sasa wajulikanao kwa Kiingereza kama "sperm whales".
 Nyangumi
Image copyright Dominica Sperm Whale Project
Image caption Nyangumi wakubwa baharini
Hadi kupatikana kwa jino hilo Beaumaris, visukuku vya nyangumi wakubwa vilikuwa vinapatikana pwani ya magharibi ya mabara ya Amerika Kusini na Amerika Kaskazini.
Makavazi hiyo imesema nyangumi mwenye jino hilo huenda alikuwa na urefu wa mita 18 na uzani wa tani 40.

soma hii: huko Kazakhstan Wabakaji wa watoto kuhasiwa.

Image copyright THINKSTOCK
Image caption Wanopenda ngono na watoto kuhasiwa Kazakhstan
Sheria mpya imeidhinishwa nchini Kazakhstan inayoruhusu utumiaji wa kemikali kuhasi ili kuwaadhibu watu waliopatikana na hatia ya kufanya ngono na watoto.
Hatua hiyo ni mojwapo ya sheria mpya kulinda haki za watoto.
Afisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Kazakhstani imesema kuwa visa vya watu wanaopenda kufanya ngono na watoto vimeongezeka kwa asilimia 50 mwaka uliopita.
Lakini wataalam wanasema kuwa kuhasi hakuna madhara makubwa ,hakudumu,hulazimika kurejelewa na ni ghali .

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...