Friday, 22 April 2016

uingereza yawatahadharisha wapenzi wa jinsia moja.


Image copyright GETTY IMAGES
Image caption Harusi ya wapenzi wa jinsia moja Uingereza
Serikali ya Uingereza imewaonya wapenzi wa jinsia moja wanaosafiri kuelekea Marekani kutokana na sheria dhidi yao katika majimbo ya North Carolina and Mississippi.
Marekani ni jamii kubwa ilio na maoni tofauti.Sheria mpya zilizopitishwa katika majimbo hayo zinaruhusu wafanyibiashara kuamua iwapo wanaweza kuwahudumia watu wa jinsia hiyo au la.
Ushauri huo umetoka katika afisi ya maswala ya kigeni ya Uingereza.
Katika jimbo la Carolina,sheria iliopitishwa na Gavana Pat McCrory inasema kuwa watu waliobadili jinsia watumie msaala wa kuogea kulingana na jinsia yao iliopo katika vyeti vyao vya kuzaliwa.
Sheria ya Mississippi pia ina sheria kama hiyo na inawalinda wafanyibiashara wengi kytoshtakiwa kwa kukataa kuwauzia wapenzi wa jinsia moja.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...