![]() |
Singida United kuumana na Mbeya City kwenye dimba la Namfua mjini Singida |
Ligi kuu Tanzania Bara inaendelea leo JUMATANO kwa kuchezwa mchezo mmoja ambapo SINGIDA UNITED waliopo kwenye nafasi ya 14 wakiwa na alama 7 itawaalika wanakoma kumwanya, MBEYA CITY waliopo kwenye nafasi ya 13 wakiwa na lama 7 pia mchezo utakaochezwa kwenye dimba la NAMFUA mjini SINGIDA.
Katika mchezo pekee uliochezwa jioni ya jana timu ya KMC na LIPULI FC zimeendelea na rekodi yake ya kupata sare kwenye michezo yao ya ligi kuu kwa msimu huu baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa UHURU jijini DSM.
Katika mchezo huo uliokuwa na mashambulizi ya kushitukiza kwa pande zote mbili ulishuhudia mlinzi wa kushoto wa LIPULI FC, PAUL NGALEMA akilimwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 90 ya mchezo huo baada ya kumchezea madhambi kiungo wa KMC, CHRIS BUYOYA.
Kwa matokeo hayo timu zote mbili zimefikisha alama SABA ambapo KMC imeshinda mchezo MMOJA na imetoka sare katika michezo MINNE na kupoteza mchezo MMOJA huku LIPULI FC wakishinda mchezo MMOJA na kutoka sare katika michezo MINNE.
No comments:
Post a Comment