Tuesday, 25 September 2018

HAMILTON jino kwa jino na VETTEL katika RUSSIAN GRAND PRIX

Lewis Hamilton anaongoza kwa tofauti ya alama 40 dhidi ya Sebastian Vettel 
Kuelekea mbio za Langalanga za RUSSIAN GRAND PRIX zitakazofanyika mjini SOCHI jumapili hii kampuni ya MERCEDES imesema haitabweteka licha ya dereva wake LEWIS HAMILTON kuongoza kwa alama 40 mbele ya mpinzani wake mkubwa SEBASTIAN VETTEL katika msimamo wa mbio hizo.

HAMILTON ameshinda mashindano MATATU kati ya MANNE yaliyopita na kujikusanyia jumla ya alama 281 akiwa kinara na kampuni ya FERARI chini ya dereva wake mashuhuri SEBASTIAN VERTEL anayeshika nafasi ya pili akiwa na alama 241 wana kibarua cha kupindua matokeo katika mashindano SITA yaliyosalia ambayo yana jumla ya alama 150.

Mtendaji mkuu wa MARCEDES, TOTO WOLFF anasema ni jambo jema kwao kuongoza msimamo mpaka hivi sasa na kwamba wapinzani wasifikiri kuwa watalegeza kamba na badala yake wataendelea kupambana zaidi.

Marcedes wanaimani kubwa ya kutetea taji la dunia

WOLFF anasema kampuni ya MERCEDES ilishangazwa na jinsi madereva wake walivyopambana katika mashindano SITA yaliyopita na kusisitiza kuwa sasa wanaweka umakini zaidi kwenye kila shindano lililkosalia ikiwemo kuhakikisha gari zinakuwa kwenye ubora wakati wote ili kutetea taji la dunaia.

Mbio za langalanga kwa msimu huu zimebakiza mashindano SITA tu kumalizika ambayo ni pamoja na yale yatakayofanyika nchini RUSSIA jumapili hii yakifuatiwa na yale ya JAPANI, MAREKANI, MEXICO, BRAZIL na ABU DHABI.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...