Monday, 11 May 2015

TANZANIA YAKUBALI KUA MWANDAAJI WA FAINALI ZA KAGAME . ONA UTAMU HUU


Mabingwa watetezi wa Kagame Cup,El-Merreikh ya Sudan.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) imekubali kuwa wenyeji wa michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati ngazi ya vilabu inayojulikana kama Kagame Cup.
Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) ambao ndio wamiliki wa mashindano haya na hutoa mialiko kwa vilabu vyenye sifa ya kushiriki. Watatoa orodha ya vilabu shiriki na ratiba ya michuano hiyo baade mwezi huu au mapema mwezi ujao.
Afisa habari wa TFF, Baraka Kizuguto amesema uamuzi wa kukubali kuwa wenyeji umetolewa na shirikisho hilo mapema Jumapili baada ya kuombwa na Cecafa.
Michuano hii inatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kuanzia tarehe 11 Julai mpaka 02 Agosti 2015.
Michuano hiyo inadhaminiwa na Raisi wa Rwanda, Paul Kagame na hufanyika kila mwaka katika nchi mwanachama za ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kati. Rwanda ndio ilikuwa mwenyeji wa michuano ya mwaka jana inayohusisha vilabu.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...