Wednesday, 3 June 2015

idadi kubwa ya tembo yatoweka tanzania. soma hii ni muhimu kuliko.

hii inasababishwa na uwindaji haramu unaofanywa na baadhi ya watanzania , tunaomba ujangili huu ukomeshwe haraka sana kwa ajili ya kuzidi kuhifadhi mali asili ya nchi ambayo ni manufaa kwa kizazi kijacho kama tulivyoikuta sisi baada ya ulindwaji mzuri wa wazee wetu waliotutangulia.



Wanaharakati wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kama janga.
Kundi linalofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.
Waziri katika serikali ya Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la Serengeti idadi yao inaongezeka .

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...