Maombolezi yanaendelea nchini kuwait kuwakumbuka watu 27 waliouawa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa kishia.
Wakati
huo huo msemaji wa kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini kuwait anasema
kuwa usalama umedumishwa katika vituo vyote vya mafuta kote nchuni humo
baada ya shambulizi ambalo Islamic State wanasema kuwa walihusika.Islamic State huwaita waislamu wa madhehebu wa shia kuwa wazushi na hivi majuzi walishambulia misikiti yao miwili katika nchi jirani ya Saudi Arabia.
No comments:
Post a Comment