Saturday, 30 May 2015

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan

Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan muda mchache uliopita
Tetemeko kubwa la ardhi limetikisa mji wa Tokyo Japan muda mchache uliopita
Tetemeko hilo ambalo linakisiwa kuwa limefikia kipimo cha 7.8 kwenye vipimo vya Ritcher limetokea takriban kilomita 874 kutoka Tokyo kusini mwa Japan.
Kulingana na idara ya uchunguzi wa ardhi tetemeko hili lilitokea saa tano u nusu na lilidumu kwa takriban dakika moja.
Majengo mengi yalitikiswa mjini Tokyo.
Hata hivyo hakuna taarifa zozote za uharibifu wala maafa kufikia sasa.
Tutakujuza zaidi kadri tutakavyopata habari zaidi.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...