Saturday, 30 May 2015

Waliokufa kwa joto India wazidi 2000 ,jinee hapa joto lilivyokua baya.


Taarifa ya Habari za Ulimwengu kutoka Idhaa ya Kiswahili ya DW

Habari | 30.05.2015 | 


Idadi ya watu waliokufa kutokana na joto kali linaloendelea kuikumba India imepindukia 2000 leo, huku maafisa nchini humo wakisema hali hiyo itaendelea kwa siku mbili zijazo. Wengi wa wahanga wameripotiwa kutoka majimbo ya kusini ya Andhra Pradesh na Telangana, ambayo wiki iliopita yameshuhudia viwango vya juu kabisa vya joto kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 12. Maafisa wa idara ya majanga wamesema zaidi ya watu 200 wamefariki tangu jana mchana, na kufanya idadi jumla ya vifo katika majimbo yote kuwa 1,979. Watu wengine 62 wameripotiwa kufariki katika majimbo ya Orissa, Mandhya Pradesh na Gujarat, na pia katika mji mkuu wa New Delhi. Viwango vya joto katika maeneo mengi vilikuwa kati ya nyuzi joto 40 na 45 za Celsius.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...