Matamshi
ya waziri wa maadili nchini Uganda kuwa Waganda wengi hujihusisha na
vitendo vya kufanya mapenzi hasa wakati wa kipindi cha mlo wa mchana
yamezua gumzo kali katika vyombo vya habari nchini humo na katika
mitandao ya kijamii.
Simon Lokodo ameongeza kusema wamiliki wa
nyumba za kulala wageni wakamatwe kwa kuwaruhusu wafanyi kazi wanaotoka
maofisini wakati wa mchana na kwenda kula uroda vyumbani humo.Wengi wanakiri kuwa tetesi hizo zimeenea nchini humo kwamba wengi wa wafanyikazi hutumia fursa ya mapumziko ya mchana kujihusisha na vitendo vya ngono na makahaba au wapenzi wao wa pembeni.
Baadhi wanaunga mkono kauli hiyo ya waziri lakini wengine wamemtaka asijihusishe na maisha ya wengine
No comments:
Post a Comment