Utawala wa Rais Barack Obama wa Marekani unafanya mipango ya
kuanzisha kambi mpya ya kijeshi katika jimbo la Anbar nchini Iraq na
kuwatuma wanajeshi wa kutoa mafunzo na ushauri kuliimarisha jeshi la
Iraq ambalo limekuwa likipambana na wanamgambo wenye itikadi kali wa
kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS. Duru zinaarifu kuwa Rais Obama
huenda akauidhinisha mpango huo wa kuongeza shughuli za kijeshi nchini
Iraq hii leo. Wanamgambo wa IS waliuteka mji mkuu wa jimbo la Anbar wa
Ramadi mwezi uliopita na Marekani inapanga kuweka mikakati madhubuti
kuukomboa mji huo. Marekani ina wanajeshi 3,100 nchini Iraq wanaotoa
mafunzo na ushauri hivi sasa. Rais Obama anatarajiwa kuidhinisha mpango
huo wa kutuma majeshi zaidi nchini Iraq mapema iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment