Tuesday, 17 June 2014

MWIMBAJI WA NYIMBO ZA DINI KIZIMBANI KWA UBAKAJI WA MFANYAKAZI WA NDANI (HOUSEGIRL)

MUME wa mwimbaji Flora Mbasha ,
Emmanuel Mbasha (32 ), amefikishwa katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es
Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili
ikiwemo ya ubakaji .
Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara
na mwimbaji alisomewa mashitaka yake
mbele ya Hakimu Mkazi, Wilberforce
Luago.
Wakili wa Serikali , Nassoro Katuga alidai
kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo
mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini
Dar es Salaam.
Katuga alidai katika shitaka la kwanza
kuwa , Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata
Kimanga, Wilaya ya Ilala , jijini Dar es
Salaam, kinyume cha sheria huku akijua ni
kosa alimuingilia kwa nguvu msichana
anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina
limehifadhiwa).
Katika shitaka la pili , ilidaiwa kuwa Mei 25,
mwaka huu eneo la Tabata Kimanga , jijini
Dar es Salaam, kinyume cha sheria ,
mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu
mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).
Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka
hayo.
Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna
pingamizi la dhamana.
Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana
kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ,
mmoja awe mtumishi wa serikali na
mwingine kutoka taasisi inayotambulika
watakaosaini hati ya dhamana ya Sh.
milioni tano .
Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya
dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi
iliahirishwa
hadi Juni 19 , mwaka huu itakapotajwa .
Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari
polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la
Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza
maisha mapya mahabusu ya Keko , jijini
Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...