Wednesday, 18 June 2014

SHAMBULIZI LA BOMU LATOKEA NIGERIA WAKATI WASHABIKI WAKITAZAMA MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA JANA JUMANNE

Shambulizi la bomu la kujitoa mhanga,
limetokea kaskazini mwa Nigeria katika eneo
la Yobe ndani ya ukumbi ambao mashabiki
walikuwa wamejaza kutazama mechi za kombe
la dunia.
Hali ya tahadhari ilitangazwa katika majimbo
matatu ikiwa ni pamoja na Yobe huku
washukiwa wa mashambulizi hayo wakiwa ni
kundi la wanamgambo wa Boko Haram.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema
mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikuwa
ndani ya gari ndogo iliyokuwa imetegwa bomu
wakati watu wakiangalia mechi kati ya Brazil
dhidi ya Mexico Jumanne jioni.
Ukumbi ambao mashambulizi yamefanyika ni
maarufu sana na mara nyingi watu wengi
hupenda kwenda kuangalia matukio makubwa.
Hata hivyo, mamlaka nchini Nigeria ilitoa
onyo kwa wakazi katika baadhi ya maeneo
kuepuka kukaa sehemu za mkusanyiko kipindi
hiki cha kombe la Dunia wakiogopa
mashambulizi ya wapiganaji.
Wachambuzi wanasema kuwa vikundi vya
wapiganaji wa Kiislam, ikiwa ni pamoja na
Boko Haram, wameelezea mpira wa miguu
kama kitu kisichofaa katika dini ya Kiislamu.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...