Tuesday, 17 June 2014

Utahiri mpya kutoka uganda

Hii ndio njia mpya
inayotumika kutahiri wanaume
Uganda.
Wizara ya afya nchini Uganda imeanza
majaribio ya kutumia kifaa kipya kwa ajili ya
kutahiri wanaume ili kujikinga na maambukizi
ya virusi vya Ukimwi.
Kifaa hicho rahisi cha mpira kinatumika kutoa
ngozi ya mbele ya uume wa mwanaume
tofauti na mwanzo ambapo kisu kilikuwa
kikitumika kufanya shughuli hiyo.
Igalla ambaye ni baba wa watoto wawili
amefanyiwa tohara kwa kutumia njia hiyo
ambapo anasema inachukua dakika chache na
hakujihisi vibaya hata kidogo tofauti na
tohara za kimila ambapo mwanaume
hutahiriwa kwa kutumia kisu.
Wanasayansi waligundua kuwa tohara kwa
wanaume inaweza kupunguza kwa kiasi
kikubwa uwezekano wa kupata maambukizi ya
virusi vya Ukimwi.
Mbali na Uganda kifaa hicho pia kinatumika
nchini Botswana, Kenya, Mozambique, Afrika
Kusini, Zambia, Zimbabwe na nchi nyingine.
Uganda ina matumaini kuwa kifaa hicho
kiitwacho PrePex kitawahamasisha wanaume
wakubwa Uganda kwenda kufanyiwa tohara
kama sehemu ya mapambano dhidi ya
ugonjwa hatari wa Ukimwi unaosababisha vifo
vya mamilioni ya watu.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...