Tuesday, 17 June 2014

HII NDIO KAULI YA RAISI WA KENYA BAADA YA KUTOKEA KWA MILIPUKO MIWILI YA MABOMU

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa
mauaji yaliyofanywa katika mji wa Mpeketoni,
Pwani ya Kenya hayakufanywa na kundi la
wapiganaji wa kiislamu la Al Shabaab.
Kauli ya Rais Kenyatta inakuja siku moja baada
ya kundi hilo kukiri kufanya mauaji
yaliyotokea Mpeketoni Jumapili usiku.
Akitoa hotuba yake ya kitaifa, Rais Kenyatta
pia amesema maafisa wa polisi Mpeketoni
ambao walifanya uzembe hadi kutokea
mashambulizi hayo watashtakiwa.
Al Shabaab lilikiri katika taarifa kwa vyombo
vya habari kuwa ndilo lilifanya mauaji hayo
Jumatatu jioni.
Mauaji zaidi yalifanyika usiku wa kuamkia leo
licha ya taarifa ya Al Shabaab kusema kuwa
washambuliaji walioshambulia Mpeketoni
walikuwa wamerejea salama nchini Somalia.
Uharibifu mkubwa ulishuhudiwa katika mji
huo huku washambuliaji wakichoma hoteli na
kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari
waliyoyatumia kwa usafiri wao.
Kenyatta amesema kuwa kuna baadhi ya
wanasiasa wanaochochea uhasama miongoni
mwa jamii.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...