Monday, 8 June 2015

G7 yatishia kuiongezea Urusi vikwazo vya kiuchumi.



G7 yatishia kuiongezea Urusi vikwazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa, viongozi wa mataifa saba yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi Duniani-G7, wamekubaliana kuwa vikwazo dhidi ya Urusi vinafaa kuendelea.
Bi Merkel amesema hadi pale muafaka wa kukomesha mapigano nchini Ukraine utakapoheshimiwa vikwazo sharti ziendelee.
Viongozi hao wanafanya mazungumzo katika mji mdogo Ujerumani
Akiongea katika siku ya mwisho ya mkutano wa siku mbili, Merkel amesema kuwa mataifa ya G7 yalikuwa tayari kuzidishia Urusi vikwazo zaidi, iwapo hali ingeruhusu.
Kuhusu mzozo wa kifedha unaokumba Ugiriki, Bi Merkel, alionya kuwa muda uliosalia kabla makubaliano hayajatiwa sahihi ni mchache mno.
Bi Merkel pia amewataka wanachama wa G7 kuchangia hazina ya kuyasaidia mataifa maskini ambayo yanaathirika na mabadiliko ya hali ya anga
Alishauri Ugiriki kuchukua hatua madhubuti ilikunusuru sarafu ya taifa hilo.
Viongozi hao wanafanya mazungumzo katika siku ya pili ya mkutano mkuu, wenye nia ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, huku pia swala la kuongezeka kwa makundi yenye itikadi kali likijadiliwa.
Bi Merkel pia amewataka wanachama wa G7 kuchangia hazina ya kuyasaidia mataifa maskini ambayo yanaathirika na mabadiliko ya hali ya anga.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...