Mshambuliaji wa Brazil Neymar atakosa michuano yote ya kombe la Copa America baada ya kupigwa marufuku ya mechi nne.
Mchezaji
huyo wa miaka 23 kutoka kilabu ya Barcelona alionyeshwa kadi nyekundu
kwa kuzozana na wachezaji wa Colombia baada ya Brazil kushindwa na
Colombia 1-0 katika mechi ya makundi.Lakini shirikisho la soka la Marekani ya kusini limekiangazia tena kisa hicho na kuongeza adhabu hiyo.
Vyombo vya habari vya Brazil vinasema kuwa alimkaripia refa kabla ya kuingia katika chumba cha mapumziko.
No comments:
Post a Comment