Sunday, 7 June 2015

Barcelona walivyochukua kombe la uefa kwa kuwafunga Juventus 3-1 juzi















barcelona walitawazwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya tano baada ya kuichapa Juventus mabao
 matatu kwa moja katika mechi kali ya fainali iliochezwa katika uwanja wa Olimpiki wa Berlin.
Barcelona walikuwa wa kwanza kufunga kupitia Ivan Rakitic kunako dakika ya nne ya mwanzo wa kipindi cha kwanza.











Hatahivyo Alvaro Morata alisawazisha .Lakini Luis Suarez alifunga bao jingine baada ya kipa Gianluigi Buffon kuutema mpira naye nyota Neymar akafunga udhia baada ya gusa ni guse kati yake na Messy.
Katika mechi hiyo Andre Iniesta ndiye aliyetangazwa mchezaji bora.

Berlin  ii inamaanisha kwamba Barcelona wameshinda mataji matatu ikiwemo lile la Copa Del Rey,La liga na la vilabu bingwa barani Ulaya.
Mechi hiyo pia ilikuwa ya mwisho kwa kiungo wa wakati wa Barcelona Xavi Hernandez ambaye anaondoka kilabu hiyo baada ya kuichezea kwa mda mrefu.











No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...