Tuesday, 11 August 2015

Wapiganaji wa Kikurdi washambuliwa na uturuki



Makabiliano kati ya wanajeshi wa Uturuki na wapiganaji wa PKK
Uturuki imeanzisha tena msururu wa mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kikurdi yanayolenga maeneo 17 kusini mashariki, kwa mujibu wa jeshi
Maeneo hayo yapo mkoani Hakkari katika mpaka na Iran pamoja na Iraq.
Uturuki imushuhudia ghasia zaidi katika wiki za hivi karibuni kati ya wanajeshi na wapiganaji wa Kikurdi wanaotaka kujiondoa.
Mashambulio hayo yanajiri siku moja baada ya watu tisa kuuawa katika msururu wa mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama, wengine wakiwa katika eneo la kusini mashariki.
Mashambulizi ya jumatatu yanalaumiwa kutekelezwa na kundi la wakurdi la PKK.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...