Saturday, 24 October 2015
Saturday, 3 October 2015
mgomo wa Walimu wasitishwa huko nchini kenya
Mgomo wa walimu nchini Kenya hatimaye umesitishwa.
Walimu sasa watarudi shuleni ili kuendelea kufunza siku ya jumatatu.Katibu mkuu wa KNUT Wilson Sossion amesema kuwa muungano huo hatahivyo hautaondoa kesi ambapo tume ya huduma za walimu TSC imekataa rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa kuwapatia walimu hao nyongeza ya mishahara ya kati ya asilimi 50-60
Hatua hiyo ya muungango wa walimu nchini Kenya KNUT inatokana na agizo lililotolewa na Jaji Abuodha mnamo tarehe 25 mwezi Septemba.
Mgomo huo ulikwamisha masomo nchini Kenya huku walimu wakitaka nyongeza ya mishahara pamoja na ile ya marupurupu.
Walimu sasa wanaitaka tume ya kuajiri walimu TSC kuwapatia mishahara ya mwezi Septemba baada ya tume hiyo kusema kuwa haitawalipa kwa kuwa walikuwa katika mgomo.
Hatua hiyo inatoa afueni kwa wanafunzi wa shule za uma ambao walilazimika kukaa nyumbani kwa kipindi chote cha mgomo huo.
''Kwa maslahi ya watoto wetu katika shule za umma na haki zao chini ya katiba mpya,mahakama imeagiza miungano hiyo ya walimu kuahirisha mgomo huo ulioanza terehe mosi mwezi Septemba kwa siku 90,ili wanachama wake waanza kazi mara moja'',alisema jaji Abuodha.
Mda mfupi tu baada ya agizo hilo kutolewaserikali ilitangaza kuwa shule zote zitafunguliwa sikuya jumatatu na kufungwa mnamo tarehe 20 mwezi Novemba
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...