Michezo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji Cup itaanza kutimua vumbi leo huko Adis Ababa Ethiopia.
Timu ya taifa ya Uganda the cranes itakuwa dimbani kukabiliana na wanyasa Malawi , huku timu ya Tanzania bara maarufu kama The Kilimanjaro stars na Wenyeji Ethiopia.
Robo fainali ya pili itapigwa hapo jumanne Desemba mosi kwa Sudan kusini kukipiga na Sudan,Rwanda wakipepetana na Kenya.
Michezo ya nusu fainali itafanyika siku ya Alhamisi huku mchezo wa fainali na ule wa kumsaka mshindi wa tatu ikifanyika siku ya jumamaosi Desemba 5.
10:33 Ndege ya Papa Francis imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Fiumicino, Roma, ikiwa imechelewa kwa karibu robo saa. Anatarajiwa kuwasili uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta saa 17:00.
10:00 Hujambo! Karibu tukupashe yanayojiri katika ziara ya Papa Francis barani Afrika ambayo itamfikisha Kenya, Uganda na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
12.06am:Marais na viongozi mbalimbali waliowasili katika hafla hiyo watambulishwa kwa wananchi waliojaa katika uwanja huo.
Image caption
Magufuli akiingiauli
12.00am:Na sasa kamanda wa jeshi anaomba rukhsa ya kuondoka uwanjani. 11.56am:Ndege za kijeshi zinapita juu ya uwanja wa Uhuru kutoa heshima kwa rais mpya wa taifa hilo John Pombe Magufuli. 11.27am:Rais Magufuli alikagua gwaride la heshima 11.23am:Mizinga 21 ya kumkaribisha rais mpya wa Tanzania John Pombe Magufuli yapigwa 11.22am:Jeshi laomba rukhsa kutoka kwa rais mpya wa Taifa la Tanzania John Pombe Magufuli
Image caption
Jukwaa la kula kiapo
11.20am:Jakaya Mrisho Kikwete sasa awasalimia viongozi waliofika katika jukwaa la waheshimiwa wakiwemo marais mbalimbali.
Image caption
Kikwete
11.18am:Sasa jeshi lamuaga aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete na aliyekuwa makamu wake Gharib Bilal 10.55am:Makamu wa rais wa Kwanza mwanamke nchini Tanzania Samia Suluhu Hassan aapishwa 10.51am:Rais mpya wa Tanzania apewa mkuki na ngao ya ishara ya kuchukua madaraka. 10.48am:''Mimi
John Pombe Magufuli naapa nitatenda kazi zangu za urais kwa mujibu wa
sheria na mila na desturi za muungano wa Tanzania,ewe mwenyezi mungu
nisaidie'' 10.47am:Rais mteule John Pombe Magufuli aapisshwa .Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pia amewasili hapa.
Image caption
Bendera
10.45am:Na sasa aliyekuwa rais wa
taifa hilo Jakaya Kikwete amekuwa raia wa kawaida baada ya bendera ya
utawala wake kushushwa hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam 10.40am:Wimbo wa Taifa la tanzania wapigwa na baadaye bendera ya rais Kikwete itashushwa ili kuashiria mwisho wa uoingozi wake. 10.39am:Mizinga 21 ya kutoa heshima za mwisho kwa rais Jakaya Kikwete yapigwa.
Image caption
Kikwete akizunguka uwanja
10.21am:Gari la gwaride la kijeshi
lililombeba rais Kikwete sasa lauzunguka uwanja huo huku wananchi
waliojjaawa na furaha wakimsalimia kwa kumpungia mkono. 10.20am:Na
sasa msafara wa Rais Jakaya Kikwete wawasili katika uwanja wa Uhuru
.KIkwete baadaye anaonekana kuingia katika gari rasmi la gwaride katika
uwanja wa uhuru na kuwapungia mkono maelfu ya wananchi waliojaa katika
uwanja huo. 10.15am:Rais Mteule John Pombe Magufuli awasili katika sherehe hizo na kulakiwa na jaji mkuu Othman Chande.
Image caption
Uwanja wa Uhuru
9.48am:Rais wa Rwanda Paul Kagame
anawasili katika uwanja wa uhuru na kuketi bega kwa bega na waliokuwa
marais wa taifa hilo Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.
9.47am:Rais
wa kisiwa cha Zanzibar Dokta Ali Mohammed Shein amewasili katika uwanja
wa Uhuru na anaonekana hapa akisalimiana na rais mstaafu wa Tanzania
Hassan Mwinyi.Kumbuka kiongozi huyo wa Zanzibar aliongezewa mda wa
kuhudumu katika kisiwa hicho baada ya tume ya uchaguzi kufutilia mbali
matokeo ya uchaguzi wa urais katika kisiwa hicho. 9.43am:Rais mteule John Pombe Magufuli atakuwa rais wa awamu ya tano kuchaguliwa nchini Tanzania tangu taifa hilo lijipatie Uhuru.
9.39am:Vilevile aliyekuwa waziri
mkuu nchini Kenya Raila Odinga ambaye ni rafiki mkubwa wa rais mteule
John Pombe Magufuli,rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph
kabila pamoja na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ni baadhi ya viongozi
waliowasiliili kuhudhuria sherehe hiyo ya kihistoria.9.35am:Miongoni
mwa viongozi wanaotarajiwa katika hafla hii ni pamoja na rais wa Kenya
Uhuru Kenyatta ambaye tayari ameondoka katika uwanja wa Jomo Kenyatta
Jijini Nairobi akiandamana na Mkewe bi. Margeret Kenyatta na anatarajiwa
kuwasili katika uwanja wa sherehe hizi wakati wowote kutoka sasa 9.30am:Gwaride
la kijeshi tayari limejiandaa vilivyo ikiwemo wanajeshi waliovalia sare
za rangi tofauti hapa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Image caption
Mapambo
8:00 am Mataifa mbalimbali yamekuwa yakituma risala za pongezi kwa Tanzania na kwa Rais Mteule John Magufuli.
Wa kwanza kutuma risala za pongezi walikuwa ni:
Rais wa Rwanda Paul Kagame na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Saharawi Mohammed Abdelaziz.
Katika
salamu zake kwa Rais Mteule Magufuli, Bw Kagame amesema: "Kufuatia
kuchaguliwa kwako kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda
kukutumia Mheshimiwa salamu za dhati, pongezi na heri nyingi kwa niaba
yangu mwenyewe, Serikali yangu na wananchi wa Rwanda.”
Naye Rais
Abdelaziz amemwambia Rais Mteule Magufuli: “Sisi tuna uhakika kuwa chini
ya uongozi wako wa busara, Tanzania itaendelea kusonga mbele na kupata
maendeleo na ustawi mkubwa zaidi.” 7:10 am
Viongozi wa baadhi ya mataifa ya Afrika wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo
Jacob Zuma kutoka Afrika Kusini, Robert Mugabe kutoka Zimbabwe na
Filipe Nyusi wa Msumbiji. Mhubiri mashuhuri kutoka Tanzania TB Joshua
pia atahudhuria sherehe hiyo. 7:00 am Watumbuizaji wanaotarajiwa kutumbuiza wakati wa sherehe walifika uwanjani mapema na ala zao.
6:45 am Uwanja umeanza kujaa watu.
Wengi wa waliofika mapema wanafurahisha kujipiga, kupigana na kupigwa
pichwa kuweka kama kumbukumbu za siku hii.
Image caption
Baadhi ya waliofika wamevalia mavazi yenye rangi za chama tawala CCM
6:30 am Uwanja wa Uhuru umepambwa ukapambika
Image caption
Uwanja wa Uhuru
6:30 am Waandishi wa BBC wamo katika uwanja huo kukuletea habari kadiri zinavyochipuka.
6:30 am Sherehe ya kumuapisha Bw Magufuli inafanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Image caption
Usalama umeimarishwa katika uwanja huo
6:00 am. HABARI YA ASUBUHI?
Rais
Mteule wa Tanzania John Pombe Magufuli anaapishwa leo kuwa rais wa
awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kutangazwa
mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Oktoba 25.
Bw Magufuli alipata asilimia 58.46 ya kura zilizopigwa kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania.