Thursday, 18 February 2016

Watu 28 wauawa katika mlipuko Uturuki,soma tazama picha za tukio


ShambulioImage copyrightEPA
Image captionHakuna kundi lililodai kuhusika
Watu zaidi ya 28 wamefariki baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara Jumatano jioni, maafisa wa Uturuki wamesema.
Watu 61 wamejeruhiwa.
Gar lililojaa vilipuzi lililipuliwa mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita, kwa mujibu wa afisi ya gavana wa Ankara.
Mlipuko huo ulitokea karibu na Bunge na makao makuu ya jeshi ya Uturuki.
Naibu waziri mkuu Bekir Bozdag amesema hicho ni “kitendo cha ugaidi”.
ShambulioImage copyrightGetty
Image captionMlipuko huo ulisikika kote mjini
Moshi ulitanda angani kutoka eneo hilo na watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mlipuko huo ulisikika kote katika mji huo.
Baadhi ya waliofariki na kujeruhiwa walikuwa raia.
Hakuna kundi lililodai kuhusika kufikia sasa

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...