Wednesday, 18 May 2016

HIVI PUNDE: Ndege ya Misri yapotea ikitoka Paris


  • Saa moja iliyopita
NdegeImage copyrightAFP
Image captionMwezi Machi ndege nyingine ililazimishwa kuelekea Cyprus
Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.
Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.
Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri.
Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga.
Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...