Monday, 23 May 2016

soma hii: Milipuko mikubwa yauwa watu wengi huko Syria hivi leo



Image copyrightAFP
Image captionAssad
Takriban watu 65 wamefariki katika milipuko ya mabomu kadhaa katika maeneo muhimu ya pwani yanayodhibitiwa na serikali ya Syria ,ripoti zinasema.
Milipuko ilikumba miji ya Tartus na Jableh.
Milipuko kadhaa ilisababishwa na walipuaji wa kujitolea muhanga,kundi moja la uchunguzi limesema.
Vyombo vya habari vya Syria vinasema kuwa vituo vya mabasi ni miongoni mwa maeneo yaliolengwa .
Image copyrightREUTERS
Image captionNgome za Assad zalipuliwa
Hospitali moja pia inadaiwa kushambuliwa.
Mashambulio kama hayo si kawaida katika eneo hilo.Hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza milipuko hiyo.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...