Image copyrightREUTERSImage captionHillary Clinton
Maafisa wa upelelezi nchini Marekani wamesema kuwa programu ya komputa inayotumiwa na jopo linalosimamia kampeni ya Bi Hillary Clinton imedukuliwa.
Mameneja wanaosimamia kampeni ya Bi Clinton walisema kuwa wadukuzi hao wameingilia mawasiliano katika kompyuta hiyo.
Awali kamati ya jopo hilo inayosimamia ukusanyaji pesa za kampeni ilisema kuwa mawasiliano yake yalikuwa yamedukuliwa.
Vyombo vya habari Marekani vinasema kuwa udukuzi huo huenda unahusika na shughuli za upelelezi za Urusi.
Image copyrightAPImage captionHillary Clinton
Shirika la upelelezi la Marekani la FBI nalo linasema kuwa linaendelea na uchunguzi kuona iwapo makundi mengi zaidi yanaendesha udukuzi huo dhidi ya kompyuta za chama cha Democratic.
Juma lililopita mtandao wa kufichua habari za siri wa Wikileaks, unaodhaniwa kuwa na uhusiano mkubwa na Urusi ulifichua barua pepe nyingi kuhusiana na chama cha Democratic.
Image captionEric Aniva 'Fisi ' mtajika aliyewabikiri zaidi ya watoto 104
Katika tamaduni nyingi kote duniani mwanamke anapoolewa huwa ni fahari kubwa sana akiwa ni bikira.
Mathalan ni dhihirisho la mwanamke kuwa amelelewa na kutunzwa vyema.
Ni dhihirisho la usafi.
Hata hivyo jamii moja nchini Malawi haithamini ubikira wa watoto wao wa kike.
Amini usiamini wazazi huwa wanamlipa ''Fisi'' kumbikiri binti yao punde tu anapopata hedhi yake ya kwanza.
Image captionAniva huchemsha mizizi hiyo kabla ya kuanza kubikiri watoto kwa takriban siku 3 hivi
Wanaamini kuwa binti ambaye ni bikira ni mkosi kwa jamii!
Malimwengu haya.
Wazazi na jamii kwa jumla katika maeneo mengi ya kusini mwa Malawi wamekuwa wakishikilia tamaduni hii kwa miaka na mikaka.
''Fisi'' ama wanaume wanaowabikiri watoto wa kike huchaguliwa na wazazi kuwaondolea mikosi.
Na huwa ni sherehe kubwa inayomtangulia binti kupelekwa unyagoni kisha kuwatembelea shangazi wake kabla ya kujulishwa kwa fisi.
Amini usiamini hao mafisi hulipwa takriban dola $7 kwa kila kitendo cha ngono na hao mabinti ambao wengi huwa na kati ya umri wa miaka 11-14.
Fisi mmoja katika kijiji cha Nsanje, Eric Aniva ameiambia BBC kuwa hajui kwa kweli amewabikiri wasichana wangapi, kwa sababu ni wengi.
''Kwa kweli mimi nimewabikiri zaidi ya wasichana 104," amesema. ''Hii ndiyo tamaduni yetu''.
Image captionAniva na familia yake
''Hapa mwanamke akifiwa lazima aje kwangu nimuondolee mkosi hata kabla ya kuzikwa kwa mumewe''.
''Mwanamke akiavya mimba pia kabla hajarejelea maisha yake ya kawaida ama hata kushiriki ngono na mwanamume mwengine lazima aje kwangu nimsafishe," alisema fisi huyo.
Aniva ambaye ana umri wa takriban miaka 40 ana wanawake wawili na watoto 5.
Anasema kuwa pale anaposhiriki ngono na watoto hao huwa anapewa muda wa siku 3 hivi kumsafisha na kumuondolea mkosi.
Kulingana na tamaduni zao, ikiwa mwanamke ama binti anakataa asibikiriwe huwa wanaamini kuwa jamaa zao watafuatwa na mikosi na magonjwa.
Rais Barrack Obama
wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya
Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi
katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu
wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo
ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa
wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi. Image copyrightReutersImage caption
Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliwapiga risasi polisi kulipiza kisasi mauaji ya Alton Sterling
Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja
kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya
mtu mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge
alikouawa mtu mweusi
Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita. Image copyrightFacebookImage caption
Alton Sterling aliyeuawa na polisi mzungu pasi na kosa lolote
Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi
baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea
kwa muda mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao.
Gavin
Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji
wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika
shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling. Image copyrightReutersImage caption
Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi
baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea
kwa muda mrefu
Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video
kwenye mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi
ambapo alitoa wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais
Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya
Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la
ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi
wazungu.
Image copyrightREUTERSImage captionBinti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili.
Kwa mtazamo wa wengi radi haiwezi kupiga mti mmoja mara mbili.,,, lakini kwa mwanamke mmoja nchini India hilo ndilo lililomkuta.
Binti huyo mwenye umri wa miaka 21 amebakwa na wanaume watano kwa mara ya pili.
Image copyrightREUTERSImage captionMiaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.
Miaka mitatu iliyopita binti huyo alibakwa na wanaume wao hao watano katika mji wa Bhiwani.
Sadfa ni kwamba binti huyo aliyetorokea mji tofauti wa Rohtak ulioko katika jimbo la Kaskazini la Haryana alishikwa na kubakwa tena juma lililopita.
Alikuwa akitembea barabarani kisha akatekwa nyara na watu ambao nusura wamnyonge.
Alinusurika kufa lakini alichokipitia ni cha kutamausha sana.
Image copyrightREUTERSImage captionBinti huyo alibakwa kwa mara ya pili na kutupwa kichakani.
Binti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.
Kwa bahati nzuri msamaria mwema aliyekuwa akipita eneo hilo alimsikia akitoa sauti hafifu na kumpeleka hospitalini alikotibiwa hadi akarejesha afya yake.
Alipopata afueni alisema maneno yaliyoibua hasira miongoni mwa jamii.
Image captionBinti huyo alibakwa na kutupwa kichakani.
Nilishtuka na kuhofia maisha yangu. Walishika na kujaribu kuninyonga.walinieleza kuwa watawaua babangu na kakangu.''
Image captionMamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.
Sijui walikonipeleka kwa sababu nilipoteza fahamu ila ninachokijua ni kuwa walikuwa wale wale walionibaka miaka mitatu iliyopita.'' binti huyo kutoka jamii maskini aliiambia runinga moja ya kitaifa nchini India.
Familia yake inasema kuwa washukiwa hao walikuwa wakiwashinikiza kukomesha mashtaka dhidi yao lakini binti yao akakataa kata kata.
Sasa polisi wametumwa huko kuwasaka watuhumiwa hao.
Mamia ya wenyeji wa mji wa Rohtak, wameandamana wakitaka serikali iwachukulie hatua kali washukiwa hao wa kosa hilo la kinyama.