Monday, 26 May 2014


Raia wenye hasira wawashambulia Bey na Jay Z kwa kuikacha harusi ya Kanye.t.



Kanye-West-famous-friendss
Hii ishu inaonekana kuwa imewagusa watu wengi sio Kim na Kanye peke yake kwasababu mashabiki wenye hasira hivi sasa wameamua kutowaacha hivi hivi na kuwashambulia wanandoa Queen Beyonce na mumewe Jay Z kwa kutofika katika harusi ya Kim Kardashian na Kanye West mjini Florence Italia.
Kupitia mitandao ya kijamii “fans” hao hawakubaki nyuma kuandika wanachojisikia juu ya kitendo hicho ambacho wamesema si uungwana kwa Jay Z kumfanyia hivyo mshkaji wake wa kitambo ambaye ni kama familia kwake kwani sio kweli kwamba yuko juu zaidi yake.
Fans
Awali taarifa zilisambaa na kudai kuwa Jay Z hawezi kuhudhuria harusi ya Kanye kwasababu itarekodiwa na kurushwa katika kipindi cha Keeping up with the Kardashians lakini baadae Info nyingine zikaja kuwa atakuwepo kwenye harusi hiyo kama msimamizi lakini mwisho wa siku hakufika kabisa.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...