Wednesday, 23 July 2014

HII HAPA ILE LIST YA WALE MASTAA WA MADRID WATAOKUJA TANZANIA SOON AS POSSIBLE.

VODACOMA Tanzania ni miongoni mwa
makampuni yaliyojitokeza kudhamini
ziara ya magwiji waliocheza kwa
mafanikio makubwa katika klabu ya
Real Madrid.
Kikosi cha magwiji hao maarufu kama
`Real Madrid Legends` kitafanya ziara
ya siku nne nchini kuanzia Agosti 22
mwaka huu na kitacheza mechi moja
ya kirafiki dhidi ya kikosi maalumu
cha nyota wa Tanzania.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari katika hoteli ya New Afrika,
jijini Dar es salaam, meneja wa ziara
hiyo, Dennis Ssebo amesema  mbali na
Vodacom, wadhamini wengine ni
Fastjet, Tropical, Pembe Flower, Lake
Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari
Beach.
Ziara hiyo ni mwaliko wa kampuni ya
Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini
ya mkurugenzi wake mkuu, Farough
Baghozah na meneja wa ziara hiyo ni
Dennis Ssebo.
Wachezaji wa Real Madrid waliocheza
La Liga miaka ya nyuma, ligi ya
mabingwa kombe la dunia kama vile
Mfaransa Zinedine Zidane, Mreno Luis
Madeila Figo na Mbrazil Ronaldo de
Lima watakuwepo katika ziara hiyo.
Ssebo kabla ya mkutano wa leo,
aliuambia mtandao huu kuwa
maandalizi ya ziara hiyo yanakwenda
vizuri na itakuwa fursa pekee kwa
Watanzania kuiona Real Madrid kwa
mara ya kwanza barani Afrika.
“Ninaloweza Kusema ni kwamba,
Watanzania wakae tayari kupokea
wachezaji 27 wa zamani wa timu ya
Real Madrid na mashabiki 23  kutoka
Hispania wanaokuja kuwashangilia
magwiji wao. Kwahiyo jumla
tunapokea watu 50 kutoka Hispania
kwa ajili ya ziara hii”. Alisema Ssebo.
“Ni ziara ambayo tulifikiria itakuwa
fupi, lakini wenzetu kumbe
wameipenda nchi na wanaifahamu,
kwahiyo ni ziara ambayo itachukua
takribani siku nne”. Aliongeza

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...