Wednesday, 23 July 2014

KOCHA MPYA WA BRAZILI ATANGAZWA LEO. Ni yule kipenzi cha wengi

Shirikisho la soka la Brazil CBF,
limemtangaza aliyekuwa mchezaji wa
Brazil, Dunga kuwa kocha wa timu ya taifa
kwa mara ya pili.
Dunga aliyeiongoza Brazil kutwaa kombe
la dunia la mwaka wa 1994 aliwahi pia
kuwa kocha katika mwaka wa 2006 hadi
2011. Dunga amechukua nafasi ya Luiz
Felipe Scolari, ambaye alijiuzulu kufuatia
kimbunga cha mabao 7-1 ambayo timu
hiyo ililazwa na Ujerumani katika hatua ya
nusu fainali .
Scolari mwenye umri wa miaka 65
aliiongoza Brazil katika semi fainali za
kombe la dunia ambapo timu hiyo ilipata
kichapo kibaya cha mabao masaba kwa
moja dhidi ya mabingwa wa kombe la
Dunia Ujerumani.
Dunga amewapiku mkufunzi wa kilabu ya
Corinthians Tite,Mkufunzi wa kilabu ya
Sau Paulo Muriciy Ramalho na Vanderlei
Luxembourg ambaye aliwahi kuifunza
timu hiyo kutoka mwaka 1998 hadi
mwaka 2000.
Wachezaji wanamtaka kocha Sabella
kuiongoza timu hiyo katika kipute cha
kuwania ubingwa wa mataifa ya Amerika
ya Kusini yaani 2015 Copa America
mashindano yatakayoandaliwa huko Chile

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...