Wednesday, 30 December 2015

mvua kubwa ya El Nino kuathiri zaidi watu mwaka 2016.soma hatari hii



mafurikoImage copyrightKenya Red Cross
Image captionKenya na Tanzania ni miongoni mwa mataifa yaliyokumbwa na mafuriko

Hali ya hewa ya El Nino ambayo imekuwa ndiyo kali zaidi katika historia itazidisha hatari ya njaa na maradhi kwa mamilioni ya watu duniani 2016, mashirika ya misaada yamesema.
Hali hii ya hewa inatarajiwa kusababisha ukame baadhi ya maeneo na mafuriko kwingine.
Baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kuathirika sana yako Afrika, huku uhaba wa chakula ukitarajiwa kufikia kilele Februari.
Maeneo mengine yakiwemo Caribbea, Amerika ya Kati na Amerika Kusini yataathiriwa katika kipindi cha miezi sita ijayo.
Hali ya hewa ya El Nino, hutokana na kuongezeka kwa joto na huathiri hali ya hewa maeneo mengi. Mwaka huu hali hii imezidi na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wenye joto zaidi duniani katika historia.
Kufikia sasa, watu 31 milioni wanakabiliwa na uhaba wa chakula Afrika, theluthi moja kati ya hawa wakiwa Ethiopia.
Inakadiriwa kwamba watu 10.2 milioni watahitaji chakua cha msaada mwaka 2016.
"Tukikosa kuchukua hatua sasa, tutahatarisha zaidi maisha ya watu wasio na uwezo maeneo mbalimbali duniani,” waziri wa ustawi wa kimataifa Uingereza Nick Hurd amesema kupitia taarifa.

EthiopiaImage copyrightAFP
Image captionEthiopia imeathiriwa sana na ukame mwaka huu

Mashirika ya misaada kama vile Oxfam yameelezea wasiwasi kwamba athari za El Nino zitazidisha makali ya mizozo ya sasa kama vile vita Syria, Sudan Kusini na Yemen.
Hali ya hewa ya El Nino inatarajiwa kumalizika katikati mwa mwaka ujao.
Kuna wasiwasi kwamba hali hii huenda ikafuatwa na hali ya La Nina ambayo katika maeneo mengi husababisha ukame.
Hali kama hii ilifuata mvua kubwa 1997/98.
El Nino hutokana na kuongezeka kwa joto baharini nayo hali ya La Nina husababishwa na kushuka kwa viwango vya joto baharini.
„Inawezekana lakini bado hatuna uhakika kama kipindi kama hiki mwaka ujao tutakabiliwa na hali kinyume na ya sasa,” anasema Dkt Nick Klingaman, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza.

Wednesday, 16 December 2015

huyu hapa Mhubiri wa Canada ambae kafungwa maisha huko nchini Korea Kaskazini


LimImage copyrightReuters
Image captionBw Lim alikiri makosa yake kwenye kikao na wanahabari
Mahakama ya juu zaidi Korea Kaskazini imemhukumu mhubiri kutoka Canada kifungo cha maisha jela na kazi ngumu.
Hyeon Soo Lim, 60, aliyekamatwa mjini Pyongyang baada ya kuzuru taifa hilo Januari kwa kazi ya kibinadamu amehukumiwa kwa makosa ya “uhalifu dhidi ya dola.”
Bw Lim, ambaye ni kiongozi wa Light Korean Presbyterian Church, alikuwa ameenda kusaidia kituo cha kutunza wagonjwa, kituo cha kuwatunza watoto na kituo cha kutunza mayatima.
Mhubiri huyo kutoka Korea, anadaiwa kukiri kuhusika katika njama ya kupanga kupindua serikali na kuunda taifa la kidini.
Shughuli zozote za kidini ni marufuku nchini Korea Kaskazini.
Taifa hilo mara kwa mara huwakamata na kuwazuia wageni wanaoenda huko kwa shughuli za kidini au kimishenari.
Bw Lim alihukumiwa baada ya kesi yake kuendeshwa kwa muda mfupi na mahakama ya juu ya Korea Kaskazini.
Inadaiwa mhubiri huyo amekiri kutoa mihadhara na kusema “Korea Kaskazini inafaa kusambaratishwa na mapenzi ya Mungu”, na kusaidia Marekani na Korea Kusini kutoa usaidizi kwa wanaotoroka Korea Kaskazini.

Tuesday, 15 December 2015

Rais Obama wa marekani asema Tumeipiga IS kwa nguvu Novemba.



Image copyrightEPA
Image captionRais wa Marekani ametathimini Operesheni dhidi ya ISIL
Rais wa Marekani, Barack Obama amesema vikosi vya Marekani vinawashambulia wanamgambo wa Islamic State kwa nguvu kuliko wakati mwingine.
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari katika wizara ya ulinzi nchini humo, Obama amesema mashambulizi zaidi ya anga yametekelezwa dhidi ya kundi hilo mwezi Novemba kuliko mwezi mwingine wowote.
Muungano wa ndege za mashambulizi ya anga, wapiganaji, ndege za mashambulizi ya mabomu na ndege zisizo na rubani vimeongeza kasi ya mashambulizi ya anga na kufikia 9,000 mpaka sasa.
''Mwezi uliopita wa Novemba, tuliangusha mabomu zaidi kwenye maeneo ya ISIL kuliko mwezi mwingine wowote tangu kampeni hii ilipoanza, pia tunawaua viongozi wa IS, makamanda wao na wauaji mmoja baada ya mwingine," amesema Obama.
Hata hivyo amekiri, kuwa kutokana na mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni, jitihada zaidi zinahitajika.
''Tunatambua kuwa jitihada zinahitajika haraka. Hakuna anayejua raia wangapi wa Syria na Iraq wanaoathirika kutokana na vitendo vya kigaidi vya IS pia na familia za San Bernardino na Paris na kwingine ambako wanaomboleza vifo vya wapendwa wao,'' amesema Rais Obama.

Tuesday, 8 December 2015

mjkbgyu

mv

Kiongozi wa Al Shabaab auawa huko nchini Somalia kwa shambulio la ndege.



Image copyrightAFP
Image captionKiongozi wa Al Shabaab auawa Somalia

Kongozi mmoja wa kundi la Al Shabaab ameuawa katika shambulizi la ndege ya Marekani.
Msemaji wa makao makuu ya ulinzi ya Marekani ,Peter Cook , kifo cha Abdirahman Sandhere ni pigo kubwa kwa usimamizi na uwezo wa mashambulizi ya kundi hilo linalounga mkono wanamgambo wa Al Qaeda.
Sandhere, anayejulikana pia kama " Ukash'' anadaiwa kuuawa Jumatano iliyopita.
Al Shabaab inaendesha kampeini ya kuing'oa madarakani serikali inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa ilikilindwa na zaidi ya majeshi 22,000 wa umoja wa Afrika.
Kundi hilo limedhibitiwa katika maeneo mengi iliyokuwa ikikalia.

Image copyrightEPA
Image captionKwa mujibu wa duru za ujasusi za Marekani Al Shabaab inakabiliwa na changamoto kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa Islamic State na Al Qaeda.

Hata hivyo kuwepo kwake na tishio la amani imedhihirika kupitia mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu na vilevile katika taifa jirani la Kenya ambapo wapiganaji wake wametekeleza mashambulizi chungu nzima na kusababisha maafa makubwa.
Kwa mujibu wa duru za ujasusi za Marekani Al Shabaab inakabiliwa na changamoto kwa sababu ya ushawishi mkubwa wa Islamic State na Al Qaeda.
Marekani imekuwa ikitekeleza mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani kuanzia mwaka wa 2011.

donald Trump atakiwa kufuta kauli yake kuwa Waislamu wasiingie Marekani

  • 8 Disemba 2015

TrumpImage copyrightAFP
Image captionTrump anaongoza kwenye kura za maoni miongoni mwa wagombea wa Republican

Vigogo wa chama cha Republican nchini Marekani wamemkemea mwenzao Donald Trump, anayetaka kuwania urais kupitia chama hicho, kwa kupendekeza Waislamu wazuiwe kuingia Marekani.
Mmoja wa wanaoshindani tiketi ya kuwania urais Jeb Bush amesema Bw Trump "mwenye kasoro akilini”. Makamu wa rais wa zamani Dick Cheney naye alisema pendekezo hilo "linaenda kinyume na yote ambayo huwa tunatetea”.
Ikulu ya White House, Umoja wa Mataifa na viongozi wa Kiislamu pia wamekosoa matamshi hayo ya Trump.
Bw Trump alikuwa amesema Waislamu wengi wana "chuki” dhidi ya Marekani.
Kwenye hotuba wakati wa kampeni, aliomba "Waislamu wote wazuiwe kuingia Marekani hadi wawakilishi wa nchi wajue ni nini kinachoendelea”
Meneja wake wa kampeni alisema marfuku hiyo ingeathiri "kila mmoja” bila kubagua kama ni mhamiaji au mtalii.

TrumpImage copyrightReuters
Image captionTrump amekuwa akitoa matamshi yanayozua utata

Lakini Bw Trump aliambia Fox News kwamba haingeathiri “watu wanaoishi humu nchini (Marekani), akiongeza kuwa Waislamu wanaohudumu katika jeshi la Marekani wangekaribishwa "nyumbani”.
Matamshi hayo ya Bw Trump yalitolewa Marekani ikiendelea kuomboleza kufuatia shambulio mbaya zaidi la kigaidi kutekelezwa tangu shambulio la Septemba 11, 2001.
Wiki iliyopita, wanandoa wawili Waislamu, ambao wanaaminika kukumbatia itikadi kali, walifyatua risasi na kuwaua watu 14 na kuwajeruhi wengine 21 katika kituo cha afya San Bernardino, jimbo la California.
Bw Trump alishangiliwa sana aliporudia ahadi yake katika mkutano wa kampeni jimbo la South Carolina saa chache baada ya kutoa matamshi hayo mara ya kwanza.

Tuesday, 1 December 2015

tazama video ya kuchekesha sana ya vituko vingine vinavyotokea uwanjani.

stori kubwa ya leo , makontena yaliyopotea yanaswa na TRA ,polisi huko mbezi, tazama video na picha hapa.



IMG-20151201-WA0015
Najua bado kuna headlines kuhusu ishu ya makontena 349 kupotea bandarini Dar es Salaam na mpaka leo Jeshi la Polisi limethibitisha kuwashikilisa watu 12 kutokana na tuhuma hizo.
Kituo cha ITV wameripoti habari dakika chache zilizopita kuhusu kukamatwa kwa makontena tisa eneo la Mbezi Tanki Bovu Dar es Salaam… Jeshi la Polisiwameshirikiana na Mamlaka ya Mapato TRA kufanikisha kukamatwa makontena hayo, yanahusiana na yaliyopotea bandarini Dar?


Monday, 30 November 2015

Robo fainali CECAFA hii hapa leo, soma ratiba ya leo hapa , kilimanjaro stars ndani.


Image captionTimu ya taifa ya Tanzania
Michezo ya robo fainali ya michuano ya kombe la Cecafa Chalenji Cup itaanza kutimua vumbi leo huko Adis Ababa Ethiopia.
Image result for taifa stars 2014Timu ya taifa ya Uganda the cranes itakuwa dimbani kukabiliana na wanyasa Malawi , huku timu ya Tanzania bara maarufu kama The Kilimanjaro stars na Wenyeji Ethiopia.
Image result for tanzania

Robo fainali ya pili itapigwa hapo jumanne Desemba mosi kwa Sudan kusini kukipiga na Sudan,Rwanda wakipepetana na Kenya.
Michezo ya nusu fainali itafanyika siku ya Alhamisi huku mchezo wa fainali na ule wa kumsaka mshindi wa tatu ikifanyika siku ya jumamaosi Desemba 5.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...