Friday, 31 July 2015
Thursday, 30 July 2015
Wednesday, 22 July 2015
huyu hapa dada mjamzito anaefungiwa ndani ya geti kila siku , mimba ya miez sita sasa
Hekaheka ya leo inatokea maeneo ya Mbezi ambapo dada mmoja wa kazi za nyumbani amekuwa akifungiwa ndani ya geti lililofungwa kwa nje huku bosi wake akiwa kazini wakati ni mjamzito wa miezi sita.
Dada huyo ambaye anatokea Sumbawanga amesema amekuwa akifungiwa ndani kila siku kwa mwezi mmoja na kutakiwa kulinda nyumba wakati wa usiku.. kingine alicholalamika ni kwamba japo ana ujauzito lakini bosi wake hajamruhusu kwenda kliniki na wala hajawahi kulipwa mshahara wake.
Jirani amesema wamekuwa wakimsikia msichana huyo akiwa kila siku analia na kuamua kumuhoji ndipo walipogundua hufungiwa nje ya nyumba na bosi wake, wanadai ananyanayasika na anatia huruma kwa hali aliyonayo.
Bosi wake amesema si kweli anamlaza nje..alikuja kwake na kumkuta msichana mwingine na kukubaliana watakua wote.
Monday, 20 July 2015
Man U yasema haitaongeza mshambuliaji
Kocha
mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua
mshambuliaji mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na
Wayne Rooney.
Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine
waliobaki ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya
mshambuliaji mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya
Uturuki hivi karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.Van Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.
Sunday, 19 July 2015
diamond apata tuzo ya mtumbuizaji bora afrika . ione hapa akiwa nayo.
diamond akiwa na meneja wake bab tale na tuzo yake sliyoipata jana mtv
Mastaa waafrika waliohudhuria tuzo MTV BASE 2015 hawa hapa
Diamond Platnumz na Vanessa Mdee ndio
walikua wasanii wa Tanzania pekee waliokuwa wakiwania tuzo za MTV Base
zilizotolewa July 18 usiku hapa Durban South Africa ambako Diamond
alishinda tuzo moja kati ya tatu alizokua anawania huku Vanessa Mdee
akufanikiwa kuchukua tuzo.
Unataka kuona jinsi ilivyokua kwenye red carpet kabla ya tuzo kutolewa? endelea kutazama hizi picha hapa chini.
Mshindi wa tuzo ya Best Live Act, Diamond Platnumz akiwa na Babu Tale (wa pili kutoka kushoto) na Salam.
Abby
kutoka Choice FM (wa kushoto) alikuwa ni miongoni mwa watanzania
walioshuhudia utoaji wa tuzo za MTV Base 2015 zilizotolewa Durban.
Subscribe to:
Posts (Atom)
CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA
Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...

-
Tuzo za VMA 2014 zimefanyika na mastaa wengi walifika kwenye hilo tukio. Listi ya mastaa hao iliongozwa na familia ya Jay Z na Beyon...
-
Luca Modric mchezaji bora wa mwaka wa FIFA Wameamua kumpa,ni baada ya kumdhurumu tuzo yake ya msimu wa 2009/10,mwaka huu wameona ai...
-
Mlinda mlango wa Derby Country akipangua mkwaju wa Phil Jones Timu ya DERBY COUNTY inayonolewa na nyota wa zamani wa CHELSEA, FRANK LAM...