Mamlaka nchini Saudi Arabia inasema kuwa imewakamata zaidi ya washukiwa 430 wa kundi la Islamic State wakati wa msako wake.
Wizara
ya maswala ya ndani nchini humo inasema kuwa wanachama wa kundi hilo
walikuwa wanapanga kuzua ghasia na kwamba njama kadhaa tayari
zimetibuliwa.Mipango hiyo ni pamoja na ule unaolenga ubalozi mmoja,mauaji ya maafisa wa usalama mbali na kutekeleza milipuko ya kujitolea muhanga ndani ya misikiti.
Kundi hilo limekiri kutekeleza mashambulizi ya mabomu mongoni mwa misikiti ilio na waislamu wa madhehebu ya shia mashariki mwa taifa hilo mnamo mwezi Mei.
Watu 25 waliuawa.
No comments:
Post a Comment