Boti moja iliyokuwa imebeba abiria 23 imegongana na mtumbwi wa wavuvi na kuzama katika ziwa Victoria Magharibi mwa Kenya.
Taarifa
za awali zilikuwa zimetoa idadi hiyo kuwa 200 lakini maafisa wa usalama
nchini Kenya wamethibitisha kuwa idadi ya abiria kwenye boti hiyo
ilikuwa 23.Watu 21 wameokolewa.
Miili ya watoto wawili imepatikana ikielea kwenye ziwa hilo.
Afisa huyo ameiambia BBC kuwa waliwaokoa watu 14 walipowasili katika eneo la tukio kabla ya kuwanusuru wengine saba waliporejea mara ya pili.
Wavuvi wanne waliokuwa kwenye mtumbwi wa pili pia waliokolewa.
Kwa mujibu wa walionusurika, boti hilo lililokuwa limewabeba abiria liligonga mtumbwi wa wavuvi kisha zote mbili zikazama majini.
Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi hii leo.
Shughuli za uokoaji zinaendelea huku maafisa wa idara za serikali ya Kenya na wavuvi wakishirikiana kuwanusuru abiria hao.
No comments:
Post a Comment