Tuesday, 18 August 2015

rais Salva Kiir akataa kutia sahihi makubaliano


Salva Kiir

Serikali ya Sudan Kusini imekataa kusaini mkataba uliotarajiwa kuleta amani na kumaliza mapigano yaliyodumu nchini humo kwa zaidi ya miezi ishirini.
Hata hivyo waasi na makundi ya upinzani wamesaini kwa upande wao.
Serikali imeomba kuongezewa siku kumi na tano zaidi kushauriana juu ya mapendekezo hayo.
Waziri kutoka Uingereza anayesimamia maswala ya Afrika ameitaka serikali ya Sudan Kusini kutia sahihi mkataba huo haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa watu hawafai kusheherekea hadi pale rais Kiir atakapotia sahihi mkataba huo.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...