Saudi
Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu
na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu
watu mashuhuri kuingia eneo hilo.
Wizara
ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi
huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131.
Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.
Saudi Arabia imekana ripoti kuwa mkanyagano uliowaua zaidi ya watu 700 karibu na mji wa Mecca ulisababishwa na kufungwa kwa barabara ili kuruhusu watu mashuhuri kuingia eneo hilo.
Wizara ya masuala ya ndani ilisema kuwa madai hayo ni ya uongo na kwamba uvumi huo ulianzishwa na vyombo vya serikali Iran ambayo ilipoteza raia 131.
Iran imeilaumu Saudi Arabia kwa mkasa na ikataka wahusika wote kuchukuliwa hatua za kisheria.
Image copyrightAPImage caption
Maafisa wa shirika la msalaba mwekundu Yola
Mlipuko mkubwa
umetokea katika kambi moja ya wakimbizi wa ndani, mjini Yola, mji mkuu
wa Jimbo la Kaskazini Mashariki la Adamawa.
Mashirika ya kutoa
misaada ya dharura yamethibitisha mlipuko huo na kusema kuwa maafisa wa
polisi wameuzingira eneo hilo kwa sasa.
Mlipuko huo ulitokea katika chumba kimoja cha kuhifadhi vyakula katika kambi ya Malkohi.
Haijabainika nini kilisababisha mlipuko huo na ni wakimbizi wangapi wameathirika.
Ripoti
zinasema kuwa zaidi ya watoto 1000 walikuwa katika kambi hiyo,
iliyojengwa kuwahifadhi watu waliokimbia makwao kutokana na uasi
unaoendelea Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Maafisa wa shughuli za uokozi wametumwa katika eneo hilo huku uchunguzi ukiendelea.
kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ameridhia talaka kwa ndoa za Waumini wa Kanisa Katoliki na kuruhusu kuoa tena. hayo yanakuja baada ya changamoto mbalimbali ambazo zilikua zinalikumba kanisa hilo , papa amepitisha sheria hiyo kwa maslahi ya wakatoliki ambao walikua wakipata matatizo ya kindoa bila kupata ufumbuzi kwa miaka mingi na kubakia ndani ya ndoa bila ya upendo wa dhati ambao haumpendezi mungu, hatua hii inatajwa kua ya muhimu na ya kihistoria kufanywa na kiongozi mkubwa kama huyu duniani. kwa taarifa zaidi endelea kuingia innosam.blogspot.com
Image caption
Jaji Mkuu wa Ghana Georgina Theodora Wood atakayeongoza mahojiano
Uchunguzi
uliofanywa na mwandishi habari za uchunguzi , Anas Aremeyaw Anas
uliomchukua miaka miwili umegundua kuwa majaji pamoja na viongozi wa juu
wa mahakama nchini humo wanakula rushwa .
Anas tayari amekwisha
waandikia waraka Rais wa nchi hiyo pamoja jaji mkuu ambao nao tayari
wamekwisha andaa tume ya kuwahoji majaji wote wanaotuhumiwa.
Kwa
mjibu wa aliyeitengeneza kanda hiyo yenye urefu wa takribani saa mia
tano, ilirekodiwa kwa zaidi ya miaka miwili. Ni majuma mawili sasa tangu
Jaji Mkuu wa Ghana alipokabidhiwa nakala yake.
Rekodi hiyo inaonyesha majaji wa mahakama ndogo na za juu wakichukua hongo na kuwalazimisha wenye kesi kutoa pesa.
Anes,
Mwandishi wa habari za uchunguzi, ambaye pia ni mwanasheshia aliwafuata
majaji kuwapa hongo ili wawaachie huru watuhumiwa. Katika maeneo
mengine alijifanya mwenye kushitaki ili atoe hongo. Leo, chombo
kinachohusika na kuwaadhibu wanasheria wanaolalamikiwa kwa rushwa
kitawasikiliza majaji wote 34 wanaohusishwa na kashifa hiyo.
Tuhuma
za rushwa si mpya katika mahakama za nchini Ghana lakini ambacho
kimekuwa kikikosekana ni ushahidi madhubuti. Kwa Waghana wengi,
uchunguzi huu wa sasa ni ushahidi mzuri wa kuunga mkono malalamiko yao
ya muda mrefu juu ya rushwa katika mahakama.
Mwandishi huyo wa habari za uchunguzi anapanga kuiachia video hiyo katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana mwezi ujao.
Ripoti kutoka
nchini Yemen zinasema kuwa muungano unaongozwa na Saudi Arabia umefanya
mashambulizi ya angani kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Sanaa, siku mbili
baada ya shambulizi la waasi lililowaua wanajeshi 60.
Walioshuhudia
walisema kuwa mashambulia hayo yalilenga ngome za waasi wa Houthi na
vikosi vilivyo watiifuu kwa rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.
Ripoti zingine kutoka hospitali za mji wa Sanaa zilisema kuwa zaidi ya raia 20 wameuawa kwenye mashambulizi hayo.
Watu 1,000 nchini Sierra Leone wamewekwa kwenye karantini baada ya kugunduliwa kuwa mwanamke wa umri wa miaka 67 alifariki kutokana na Ebola.
Hilo limejiri siku tano tu baada ya kuanza kwa hesabu ya wiki sita iliyolenga kutangaza taifa hilo kuwa bila Ebola.
Karantini hiyo itadumu wiki tatu, mradi tu kusiwe na visa vipya vitakavyoripotiwa.
Watu Zaidi ya 11,000 wamefariki tangu kuanza kwa mkurupuko wa Ebola nchini Sierra Leone, Guinea na Liberia.
Mwandishi wa BBC Umaru Fofana katika mji mkuu wa Freetown, anasema maafisa wa serikali nchini humo walikuwa na matumaini baada ya kupita kwa kipindi kirefu bila kisa kipya cha Ebola na kwamba kisa cha sasa kimewashangaza.
Mwandishi wetu anasema karantini ya sasa ina masharti makali zaidi kuliko za awali. Ni pamoja na amri ya kuzuia watu kutembea kutoka nyumba moja hadi nyingine.
Wanajeshi na maafisa wa polisi wametumwa kudumisha karantini hiyo katika kijiji cha Sellakaffta, kilichoko Kambia kwenye mpaka wa kaskazini wa taifa hilo na Guinea.
Maafisa wa Shirika la Afya Duniani na wizara ya afya Sierra Leone wanapanga kutoa chanjo kwa wale ambao huenda walikutana na mwanamke huyo.
Guinea inajaribu kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa huo nchini humo. Liberia, WHO ilitangaza kuwa virusi vya Ebola vimeacha kusambaa kwa mara ya pili Alhamisi.
Taifa hilo lilitangazwa kutokuwa na Ebola mwezi Mei lakini visa zaidi vikaripotiwa mwezi uliofuata.
Image copyrightReutersImage captionBaba wa mtoto aliyekufa akataa hifadhi
Baba wa mtoto kutoka nchini Syria ambaye alikufa maji wiki hii na kuzua changamoto za kutaka kuchukuliwa hatua za kutatua suala la uhamiaji nchini syria anaripotiwa kukataa hatua ya Canada ya kumpa makao.
Tima Kurd, ambaye ni dadake Abdullah al Kurdi alisema, alimuambia kuwa anataka kusalia nchini Syria yaliko makaburi ya mkewe na wanawe wawili wa kiume ambao pia walikufa maji nje ya pwani ya Uturuki siku ya jumatano.
Image copyrightReutersImage captionBaba na watoto wake waliokufa maji
Wote hao walizikwa nchini Syria siku ya Ijumaa
Picha za mwili wa mtoto huyo wa miaka mitatu katika ufuo wa Uturuki zilizua mjadala kuhusu hatma ya watu wanaokimbia mapigano nchini Syria.
Image copyrightReutersImage caption
Wakimbizi kutoka Syria
Kamishna wa tume ya
Umoja wa Mataifa, anayehusika na masuala ya wakimbizi, Antonio
Guterres, ameyaomba mataifa ya Ulaya kuwakubali wakimbizi laki mbili
wanaokimbia mapigano nchini Syria, Iraq na Afghanistan.
Bwana Guterres amesema kuwa jibu lao huenda likaathiri mustakabali wa muungano wa Ulaya.
Kamishna Guterres amewasihi viongozi wa Ulaya kutafuta namna ya kuwaruhusu wakimbizi halali kuingia Ulaya kwa urahisi.
Kamishna
huyo wa Umoja wa Mataifa, ameonya kuwa nchi za Ulaya haziwezi kuendelea
kushughulikia suala hili la wakimbizi kila moja kwa njia yake.
Amesema
kuwa bara hilo likikosa kushikana kwa pamoja kuhusu suala hili
watakaonufaika ni walanguzi wa binadamu na mawakala wa wahamiaji. Image copyrightImage caption
Antonio Guteres
Awali wajumbe kutoka tume ya Ulaya, walianza ziara
katika kisiwa cha Kos, nchini Ugiriki, ambako maelfu ya wakimbizi
wamekuwa wakiwasili kila siku.
Wengi wa wakimbizi hao,
wamelalamika kuwa inawachukua muda mrefu, kabla ya kupata stakabadhi
wanazohitaji kuondoka kisiwani humo.
Serikali ya Ugiriki imeahidi
kuharakisha shughuli hiyo, lakini kamishna wa Ugiriki, anayehusika na
masuala ya uhamiaji amesema kuwa ni lazima mataifa yote ya Ulaya,
yashirikiane kutafuta suluhisho la kudumu.
Ziara hii ya tume ya Ulaya, ndio ya punde zaidi katika msururu wa juhudi za kutafutia ufumbuzi janga la uhamiaji barani Ulaya.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia
Miili ya wanajeshi 10 wa Uganda, waliouawa na wapiganaji wa al-Shabaab, nchini Somalia imesafirishwa nyumbani.
Msemaji wa jeshi, Kanali Paddy Ankunda, amesema shambulio hilo "limebadili mambo" na al-Shabaab wanafaa kutarajia "jibu lifaalo".
Wanajeshi 12 wa Uganda waliuawa kwenye shambulio hilo la Jumanne, kwenye kambi ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika (AU) Kusini mwa Somalia.
Al-Shabaab walisema waliua wanajeshi 70 wa AU.
Wanajeshi wa Uganda wamo kwenye kikosi cha wanajeshi 22,000 cha AU, kinachokabiliana na wapiganaji hao nchini Somalia.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia
Kwenye tamko la kwanza kabisa kutoka kwa jeshi la Uganda kuhusu shambulio hilo, Kanali Ankunda alisema kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter: "Hatutalegeza juhudi zetu za kusaidia kurejesha amani Somalia licha ya shambulio hilo." Hakutoa maelezo kuhusu miili ya wanajeshi hao wengine wawili waliouawa.
Ripoti nyingine zinakadiria wanajeshi waliouawa kwenye uvamizi huo katika kambi ya Janale, kilomita 90 Kusini Magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, ni kati ya 20 na 50.
Wakazi wanasema shambulio hilo lilianza kwa shambulio la kujitoa mhanga lililotekelezwa kwa kulipua gari lililotegwa bomu kwenye lango la kambi hiyo, na kisha kukawa na ufyatulianaji wa risasi uliodumu zaidi ya saa moja.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia ikiwasili
Licha ya kupoteza ngome nyingi kusini na kati mwa Somalia, al-Shabaab wameendelea kushambulia vikosi vya serikali na Muungano wa Afrika pande mbalimbali nchini humo.
Wapiganaji hao pia hutekeleza mashambulio ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga Mogadishu.
Image captionMilili ya wanajeshi wa Uganda waliouawa Somalia wakati ilipowasili Uganda