Monday, 2 May 2016

Maelfu ya watu watarajiwa kujitokeza kumuaga Papa Wemba.


Papa Wemba

Image copyright
Image captionMwili wa Papa Wemba utazikwa Jumatano
Maelfu ya watu wanatarajiwa kujitokeza leo mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoa heshima zao za mwisho kwa mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za rumba Papa Wemba.
Leo ndiyo ni siku ya kwanza ya kipindi cha siku tatu za maombolezo rasmi ya kumuenzi mwanamuziki huyo nchini humo.
Wemba, 66, aliyesifika kote duniani kama mmoja wa wanamuziki nguli wa nyimbo za rumba kutoka DR Congo, alifariki baada ya kuzirai akitumbuiza mjini Abidjanwiki moja iliyopita.
Alipendwa sana na mashabiki kwa nyimbo zake na pia mtindo wake wa mavazi.
Wemba

Image captionMwili wa Papa Wemba ulisafirishwa hadi Kinshasa Alhamisi
Mwanamuziki huyo, ambaye jina lake la kuzaliwa ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, anatarajiwa kuzikwa Jumatano.
Rais Joseph Kabila ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuhudhuria ibada ya wafu leo kwa heshima ya marehemu mjini Kinshasa.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...