Miili ya wakwea milima wawili kutoka Marekani waliotoweka katika milima ya Himalaya miaka 16 iliyopita imepatikana.
Mkwea
milima maarufu duniani Alex Lowe alikuwa akikwea katika kilele cha
Shishapangma chenye urefu wa 8,013m (26,290ft) eneo la Tibet Oktoba 1999
akiwa na mpiga picha David Bridges mkasa ulipotokea.Wawili hao walifukiwa na maporomoko ya theluji.
Miili yao ilionekana na wakwea milima wawili wiki iliyopita ikiwa bado imekwama kwenye theluji.
Yeye na Bridges, 29, walikuwa marafiki wakuu na walikuwa wakitafuta njia mpya ya kukwea mlima Shishapangma , mlima wa 14 kwa urefu duniani.
Mkewe Lowe, Jennifer Lowe-Anker, amesema kupatikana kwa mwili wa mumewe kutasaidia familia yake kutulia.
Jennifer baadaye aliolewa na Conrad Anker mwaka 2001.
Baadaye, yeye na wenzake wengine walitafuta wawili hao kwa siku nyingi bila mafanikio.
No comments:
Post a Comment