Tuesday, 10 May 2016

Pigo Kubwa kwa IS: Kiongozi ‘muhimu’ wa Islamic State auawa

Waheeb


Image copyrightAFP
Image captionAbu Waheeb wakati mwingine alifahamika kama Shakir Waheeb
Jeshi la Marekani limesema mmoja wa viongozi wakuu wa kundi linalojiita Islamic State ameuawa kwenye shambulio la kutoka angani.
Msemaji wa Pentagon Peter Cook amesema Abu Waheeb, ambaye amekuwa afisa mkuu wa kijeshi wa Islamic State katika mkoa wa Anbar nchini Iraq aliuawa pamoja na watu wengine watatu baada ya gari lao kushambuliwa katika eneo la Rutba.
Marekani imesema kifo cha Abu Waheeb ni pigo kubwa kwa uongozi wa IS.
Wahib alizaliwa 1986 na alikuwa mwanafunzi wa zamani wa sayansi ya kompyuta ambaye alielezwa na mitandao inayofuatilia shughuli za Islamic State kama mtu ambaye nyota yake katika kundi hilo ilikuwa iking’aa.
Alikamatwa na wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na kuhukumiwa kifo lakini akatoroka jela mwaka 2012.
Mwaka uliofuata, alishiriki katika mauaji ya kundi la madereva wa malori kutoka Syria yaliyokuwa yakipitia Iraq.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...