Saturday, 21 May 2016

waziri afutwa kazi na rais kwa kuwa mlevi, mtazame hapa.


Image captionYaripotiwa kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.
Waziri wa mambo ya ndani nchini Tznania Charles Kitwanga amefutwakazi kutokana na sababu ya kuwa mlevi akiwa kazini.
Kwenye taarifa, rais John Magufuli alisema kuwa bwana Kitwanga alienda bungeni na kujibu swali la mbunge akiwa mlevi.
Hata hivyo bwana Kitwanga hajasema lolote.
Image copyrightSTATEHOUSE TANZANIA
Image captionRais John Magufuli
Rais Magufuli ambaye aliingia ofisini mwaka uliopita aliahidi kupambana na ufisadi na awewafuta kazi maafisa kadha kuhusiana na suala la ufisadi.
Lakini waandishi wa habari wanasema kuwa kufutwa kwa bwana Kitwanga ni jambo la kushangaza kwa sababu amekuwa rafiki wa rais kwa siku nyingi.

No comments:

Post a Comment

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...