![]() |
Rais wa chama cha soka nchini Malawi Walter Nyamilandu |
Rais wa chama cha soka cha nchini MALAWI, WALTER NYAMILANDU amechaguliwa kuwa mjumbe wa baraza kuu la shirikisho la soka duniani FIFA atakayeliwakilisha shirikisho la soka barani CAF katika uchaguzi uliofanyika pale SHARM El SHEIKH nchini MISRI.
NYAMILANDU amepata kura 35 na kumshinda DANNY JORDAAN ambaye ni rais wa chama cha soka nchini AFRIKA KUSINI aliyepata kura 18 baada ya mizunguko miwili ya upigaji kura kukamilika.
![]() |
Rais wa zamani wa TFF Leodgar Tenga alishindwa kwenye uchaguzi huo |
Katika uchaguzi huo kulikuwa na mizunguko mitatu ya upigaji kura ambapo katika muzunguko wa kwanza walikuwepo wagombe watatu pamoja na aliyekuwa rais wa TFF LEODGAR TENGA ambaye yeye aliondolewa katika raundi hiyo ya kwanza.
Rais wa shirikisho la soka nchini KENYA, NICK MWENDWA na yule wa chama cha soka nchini SEYCHELLES, ELVIS CHETTY wenyewe walijitoa katika kinyang’anyiro hicho mapema kabla ya zoezi la upigaji kura katika mzunguko wa kwanza.
![]() |
FIFA ndiyo chombo chenye maamuzi ya mwisho ya uendeshaji soka duniani |
Baraza kuu la FIFA ndiyo lenye dhamana ya kuendesha na kusiamami shughuli zote za mpira wa miguu duniani na wajumbe wake hutoka katika mashirikisho ya soka kwenye mabara yote.
Uchaguzi huo umefanyika kujaza nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa rais wa chama cha soka nchini GHANA, KWESI NYANTAKYI aliyejiuzulu kutokana na kashfa ya rushwa ya dola za kimarekani 65,000 kutoka kwa mwandishi wa habari aliyejifanya ni mwekezaji wa soka.
No comments:
Post a Comment