Sunday, 28 June 2015

DOWNLOAD HII NGOMA MPYA YA JAFFARAI FT KASSIM KAMA HUJAIPATA. NI MOJA YA CLUB BANGER TAMU SANA

Aliyejilipua Kuwait huyu hapa pichani, ni raia wa Saudi


Aliyejilipua Kuwaiti ni raia wa Saudi
Vyombo vya habari nchini Kuwaiti zinasema kuwa mlipuaji wa kujitolea mhanga aliyejilipua ndani ya msikiti nchini humo Ijumaa na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 25 ni raia wa Saudi Arabia.
Katika taarifa iliyotolewa na wizara ya usalama wa ndani nchini Kuwait mshambuliaji huyo anatambuliwa kuwa ni Fahd Suliman Abdul-Muhsen al-Qabaa.
Yamkini taarifa hiyo inasema kuwa Fahd alikuwa ametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege ulioko Kuwaiti saa chache kabla yake kutekeleza shambulizi hilo la kwanza kutokea nchini humo.

 null






Aliyejilipua Kuwaiti ni raia wa Saudi Arabia 
 
Takriban watu 27 wamethibitishwa kufariki katika shambulizi hilo ambalo serikali ya Kuwaiti inasema kuwa inalenga kuchochea uhasama wa kidini baina ya Wasuni na Washia wa Kuwaiti.
Kulingana na maafisa wa uhamiaji, Fahd alikuwa nchini humo kinyume cha sheria.
Takriban watu 27 wamethibitishwa kufariki katika shambulizi hilo
Kundi la wapiganaji la Islamic State limedai kuwa Fahd Suliman Abdul-Muhsen al-Qabaa ni mmoja wao.
Kundi hilo linawakashifu waislmu washia kuwa wanakufuru na kukiuka maadili haswa na mafundisho ya mtume Muhammad.
Fahd alikuwa ametua katika uwanja wa kimataifa wa ndege ulioko Kuwaiti saa chache kabla yake kutekeleza shambulizi hilo
Mwezi uliopita tawi la Saudi Arabia la Islamic State lilitekeleza mashambulizi katika misikiti ya washia nchini humo.
Mashambulizi haya haswa kwa mataifa yanayochangia jeshi la muungano linalopigana na Wahouthi nchini Yemen na Islamic State nchini Syria na Iraq yamefikisha ujumbe wa ugaidi nyumbani kwa mataifa ya kanda hiyo ya ghuba kwa mujibu wa mwandishi wa BBC wa maswala ya Mashariki ya kati na ghuba Sebastian Usher.


 null


 null
Takriban watu 200 wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo
Takriban watu 200 wamekamatwa kutokana na shambulizi hilo lililoibua hofu miongoni mwa waislamu washia nchini humo.
Kuwait inaidadi kubwa ya washia katika kanda hiyo.

Saturday, 27 June 2015

lione gari alilopewa dogo aslay na mkubwa fella kama hukubahatika kuliona.





 aslay kwa furaha kubwa akasema haya: 

“Asante mungu Kwa kunipa uhai Na kipaji ambacho leo hii kina fanya naitwa Aslay pia nakushukuru kwa kunifikisha kwenye mikono Ya mtu mwenye moyo wa kibinaadamu. Najua kuna mengi makubwa ambayo boss wangu @mkubwafella umenifanyia ambayo si vyema kuyataja yote kwasababu wakati wake haujafikia ila naomba nichukue fulsa hii kukushukuru kwa hiki ulichonifanyia leo katika sherehe Ya kusherehekea siku yangu Ya kuzaliwa umenifanya nijione mwenye thamani kubwa duniani sikutegemea kama leo itakuwa siku yangu ya kumbukumbu ambayo sitoweza kuisahau hata Nije kuwa bilionea @mkubwafella asante kwa kunipa hii zawadi ambayo mimi kama mimi sikuiwazia kabisa kama Leo nitapata gari Na ninaushukuru uwongozi mziki Wa #mkubwanawanawe pamoja na manager wangu @chambusso boss wangu @babutale @mhtemba na mama yangu @sweatfella bila kuwasahau wasanii wenzangu wa @yamoto_band mungu





Mahakama Marekani yaruhusu ndoa za mashoga, ona wanavyoshangilia


Mahakama kuu nchini Marekani imetoa hukumu Ijumaa na kusema katiba ya nchi hiyo inatoa haki kwa wapenzi wa jinsia moja kuoana, na hivyo kutoa ushindi wa kihistoria kwa vuguvugu linalotetetea haki za mashoga.
Hukumu hiyo iliyopitishwa na majaji watano dhidi ya wanne imesema uhakikisho wa katiba wa ulinzi sawa chini ya sheria unamaanisha kuwa majimbo hayawezi kupiga marufuku ndoa za jinsia moja. Kufuatia hukumu hiyo, ndoa za jinsia moja zitakuwa halali katika majimbo yote 50 ya Marekani.
Jaji Anthony Kennedy, akiandika kwa niaba ya mahakama, amesema matumaini ya wapenzi wa jinsia moja wanaopanga kuoana ni kutengwa na kuishi maisha ya upweke, na kutenganishwa na taasisi za moja ya demokrasia za muda mrefu zaidi duniani. "Wanaomba heshima sawa mbele ya sheria. Katiba inawapa haki hiyo," amesema.
Kennedy ambaye hutoa kura ya maamuzi katika kesi katika kesi zenye mvuto mkubwa, aliungwa mkono na wengine wa majaji wanne waliberali wa mahaka hiyo. Kennedy ambaye aliteuliwa na rais Mrepublican Ronald Reagan mwaka 1988, hivi sasa ameandika hukumu zote muhimu nne kuhusu haki za mashoga, ambapo ya kwanza ilikuja mwaka 1996.
Wapinzani wa ndoa za jinsia moja wakiandamana mbele ya mahakama kuu. Wapinzani wa ndoa za jinsia moja wakiandamana mbele ya mahakama kuu.
"Bila kutambuliwa, utulivu na kutabirika kwa ndoa, watoto wao watateseka na unyanyapa wa kujua kuw afamilia zao haziko sawa na nyingine," aliandika Kennedy. Katika maoni yanayokinzana, jaji mhafidhina Antonin Scalia, alisema uamuzi huo unaonyesha kuwa mahakama hiyo ni tishio kwa Wamarekani.
Jaji mkuu wa Marekani, mhafidhina John Roberts, alisoma muhtasari wa upinzani wake kutokea nje ya chemba la majaji, hii ikiwa mara ya kwanza kwake kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 10 aliokaa katika mahakama hiyo. Roberts alisema ingawa zipo hoja za nguvu kisera katika suala la ndoa za jinsia moja, halikuw ajukumu la mahakama hiyo kuyalaazimisha majimbo kubadili sheria zake za ndoa.
Obama, Clinton washerehekea, Republican walaani
Rais Barack Obama, ambaye ni rais wa kwanza alieko madarakani kuunga mkono waziwazi ndoa za jinsia moja, alisifu hukumu hiyo, akisema kwenye mtandao wake wa twitter kuwa siku ya leo ni hatua muhimu katika safari ya kuhakikisha usawa kwa watu wote.
Naye Hillary Clinton, mgombea anaepewa nafasi kubwa kupitishwa na chama Demokratic kuwania urais mwaka 2016, aliandika kwenye mtandao wake wa twitter kuwa "Najivunia kusherehekea ushindi wa usawa wa ndoa." Hadi mwaka 2013, Clinton alisema alikuwa anapinga ndoa za jinsia moja, lakini alibadili mtazamamo wake tangu wakati huo.
Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani. Rais Barack Obama ameitaja hukumu hiyo kuwa ni ushindi wa usawa nchini Marekani.
Mgombea wa chama cha Republican Mike Hackabee alisema, uamuzi huu wa udanganyifu ni uababe wa mahakama unaokwenda kinyume na katiba." Mgombea mwingine wa Republican Jeb Bush aliongeza kuwa, " nikiongozwa na imani yangum naamini katika ndoa za asili. Naamini mahakama kuu ilipaswa kuyaruhusu majimbo yafanye uamuzi huu.
Ndoa za jinsia moja zilikuwa zinaruhusiwa katika majimbo 36 ya Marekani pamja na Washington DC. Katika jimbo la 37 la Alabama, mahakama iliondoa marufuku dhidi ya ndoa za jinsia moja, lakini mahakama ya rufaa iliwazuwia maafisa wa serikali kutoa leseni kwa wapenzi wa jinsia moja.
Wapinzani wa ndoa hizo wanasema uhalali wake unapaswa kuamuliwa na majimbo yenyewe, na wengine wanasema kuruhusiwa kwa ndoa hizo ni dharau kwa ndoa ya asili kati ya mwanamume na mwanamke, na kwamba Biblia inalaani mahusiano ya jinsia moja.
Hisia juu ya hilo zilikuwa juu wakati wa mjadala mahakamani mwezi April katika kesi hiyo, pale mwandamanaji alipowapigia kelele majaji na kuwambia wataozea jahanam ikiwa watapitisha hukumu kuunga mkono ndoa za jinsia moja.

hii ndio nyimbo pekee nyingine kutoka tanzania inayooneshwa television za marekani

kama nyimbo za mungu hii ni nzuri kupita yoyote unayoijua tanzania. ni mpya . angel benard, download hapa kwa hisani ya innosam

ona kavani alivyopigwa kidole na kuongezwa kadi nyekundu juu.

tazama video na nyimbo mpya p square kama hujaiona. nishidaaaaaaaaa kutoka marekani

tazama video ya huyu mrembo akipiga picha na kukosa pozi baada ya kitu kidogo kumzingua.











WATU 27 WAUWAWA KWA SHAMBULIO HUKO KUWAIT . ONA VIDEO NA PICHA YAKE HAPA





Kuwait yaomboleza vifo vya watu 27

Maombolezi yanaendelea nchini kuwait kuwakumbuka watu 27 waliouawa kwenye shambulizi la kujitoa mhanga kwenye msikiti wa kishia.
Wakati huo huo msemaji wa kampuni ya kitaifa ya mafuta nchini kuwait anasema kuwa usalama umedumishwa katika vituo vyote vya mafuta kote nchuni humo baada ya shambulizi ambalo Islamic State wanasema kuwa walihusika.
Islamic State huwaita waislamu wa madhehebu wa shia kuwa wazushi na hivi majuzi walishambulia misikiti yao miwili katika nchi jirani ya Saudi Arabia.







Thursday, 25 June 2015

condom zinazotambua magonjwa zaja, zione hapa



mipiraa
Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Uingereza wamezindua mipira ya kiume ‘kondomu’ yenye uwezo wa kugundua maradhi ya zinaa wakati watumiaji wanapokutana kimwili.
Kondomu hiyo inayojulikana kama S.T.EYE inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.
mipira
Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo kwa muhusika.
Kutukana na kuvumbua mipira hiyo wanafunzi hao tayari wametunukiwa tuzo ya ubunifu na kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia ya ‘the TeenTech’ pamoja na pauni 1,000.
Wanafunzi hao wamesema wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kusaidia vizazi vijavyo ili kuepukana na maradhi yanayoweza kuzuilika kitaalam
.

Wednesday, 24 June 2015

watu 18 wafa huko china leo


 



Watu wa kabila la Uigurs nchini Uchina
Ripoti za vyombo vya habari nchini Marekani zinasema kuwa watu 18 wameaga dunia katika eneo la Uchina la Xinjiang katika makabiliano na polisi katika eneo la ukaguzi.
Radio Free Asia inasema kuwa watu hao wa kabila la Uighurs walitumia visu na mabomu kuwashambulia maafisa wa polisi.
Hakujakuwa na mawasiliano rasmi kuhusu tukio hilo lakini wafanyikazi wa hospitali katika mji wa Kashgar wameiambia BBC kuwa maafisa hao wa polisi walipokea matibabu.
Moja ya lengo huenda ni kuweka vikwazo vikali kwa waislamu wa Uighurs katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadan.

watu 120 wameuwa hivi punde huko mogadishu

 

Mogadishu Somalia





Mlipuaji wa kujitolea muhanga ameligongesha gari lake na lile la kijeshi katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu na kusababisha mlipuko mkubwa.

Ripoti zinasema kwamba takriban watu 12 waliuawa na wengine kujeruhiwa wengi wakiwa raia.

Shambulizi hilo lilitokea karibu na ubalozi wa falme za kiarabu UAE
Vyombo vya habari nchini Somalia vimeripoti kwamba balozi amenusurika mlipuko huo ambao umeutaja kama jaribio la mauaji.

Tuesday, 23 June 2015

Joto kali lawaua watu 700 Pakistan


Joto kali
Waziri mkuu nchini Pakistan Nawaz Sharrif ametaka hatua za dharura kuchukuliwa huku idadi ya watu waliofariki kutokana na wimbi la joto katika mkoa wa kusini wa Sindh ikifikia 700.
Mamlaka ya kukabiliana na majanga ya dharura NDMA imesema kuwa imepokea maagizo kutoka kwa Nawaz Sharrif kuchukua hatua za dharura.
null
Joto kali
Jeshi tayari limepelekwa katika eneo hilo kujenga vituo vya kukabiliana na joto hilo ili kuisaidia mamlaka hiyo.
Wengi wa waathiriwa ni watu wazima kutoka kwa familia zinazopata mapato ya chini.
null
Joto kali
Maafisa wa afya wanasema vifo vingi vimetokea katika mji mkuu wa Karachi ambao ulikumbwa na joto la viwango vya juu vya hadi digree 45 c.
Katibu wa afya katika mkoa wa Sindh Saeed Mangnejo amesema kuwa watu 612 walifariki katika hospitali kuu ya serikali mji huo katika kipindi cha siku nne zilizopita.
null
Joto kali
Wengine 80 wameripotiwa kufariki katika hospitali za kibinafsi.

Sunday, 21 June 2015

Mapigano makali yaendelea Mogadishu Mapigano makali yaendelea Mogadishu Mapigano makubwa yameripotiwa kwenye mji kuu wa Somalia Mogadishu baada ya shambulizi la gari la kujitoa mhanga kutokea karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo. Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab waliingia jengo lililo karibu na makao hayo makuu ya ujasusi, na kukana madai ya al-Shabab kuwa waliingia makao ya ujasusi yenyewe. Hakuna ripoti zozote zilizotolewa za watu kuuawa au kujeruhiwa Al-Shabab wameapa kuongeza mashambulzii dhidi ya serikali ya Somalia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan ambao ulianza siku ya Jumatano.
Mapigano makali yaendelea Mogadishu http://ichef.bbci.co.uk/news/ws/660/amz/worldservice/live/assets/images/2015/04/20/150420095041_somalia_640x360_epa.jpg Mapigano makali yaendelea Mogadishu Mapigano makubwa yameripotiwa kwenye mji kuu wa Somalia Mogadishu baada ya shambulizi la gari la kujitoa mhanga kutokea karibu na makao makuu ya idara ya ujasusi ya nchi hiyo. Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa wapiganaji kutoka kundi la al-Shabab waliingia jengo lililo karibu na makao hayo makuu ya ujasusi, na kukana madai ya al-Shabab kuwa waliingia makao ya ujasusi yenyewe. Hakuna ripoti zozote zilizotolewa za watu kuuawa au kujeruhiwa Al-Shabab wameapa kuongeza mashambulzii dhidi ya serikali ya Somalia wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadan ambao ulianza siku ya Jumatano.

Saturday, 20 June 2015

neymar apata adhabu ya pigo baada ya kupata kadi nyekundu



 null

Neymar
Mshambuliaji wa Brazil Neymar atakosa michuano yote ya kombe la Copa America baada ya kupigwa marufuku ya mechi nne.
Mchezaji huyo wa miaka 23 kutoka kilabu ya Barcelona alionyeshwa kadi nyekundu kwa kuzozana na wachezaji wa Colombia baada ya Brazil kushindwa na Colombia 1-0 katika mechi ya makundi.
Neyma akicheza dhidi ya Colombia 
 
 
 
 
null
 
 
Alikuwa amepewa marufuku ya mechi moja ambayo ingemlazimu kukosa mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya Venezulea siku ya jumapili.
Lakini shirikisho la soka la Marekani ya kusini limekiangazia tena kisa hicho na kuongeza adhabu hiyo.

 null



Neymar akamkaripia refa
Neymar alionyeshwa kadi nyekundu baada ya kuupiga mpira kimakusudi kwa lengo la kumgonga mchezaji wa Colombia Pablo Armero baada ya kipenga cha mwisho cha mechi kabla ya kumpiga kichwa mchezaji mwengine ambaye alimsongelea.
Vyombo vya habari vya Brazil vinasema kuwa alimkaripia refa kabla ya kuingia katika chumba cha mapumziko.

maafisa 15 wa usalama wauwawa na al shabab . hawa jamaa ni hatari sana






 
Al Shabaab
Wanamgambo wamewaua karibu walinda usalama 15 nchini Somalia baada ya kufanya shambulizi katika mji ulio karibu na mji mkuu Mogadishu.
Maafisa wanasema kuwa wanamgambo wa Al Shabaab kwanza walishambulia kizuizi cha polisi cha Afgoye ambapo waliwaua polisi watatu na kuchukua magari kadha.
Kisha waliwavamia na kuwaua wanajeshi kadhaa.
Al Shabaab wanasema kuwa wameongeza mashambulizi siku za hivi majuzi kwa sababu ni mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Friday, 19 June 2015

BAADA YA KUISHA KWA NDOA YAO ONA MALI ZINAVYOPASULIWA NUSU KWA NUSU


divorce-half-of-everything-12
Ni kama utani hivi.. eti kweli ikitokea ndoa inaisha alafu Mahakama ikaamua kila kitu mgawane nusunusu, hiyo nusu yenyewe ndio inakuwa kwenye mtindo huu??
Der Juli ni jina la Mjerumani mwingine kwenye Headlines baada ya kuingia mtandaoni na kutangaza kwamba anauza hivi vitu ambayo wamegawana nusunusu na mkewe baada ya ndoa kufikia mwishoni.
Cheki pichaz za vitu vyewewe sasa !!
half-a-macbook-pro-der-juli-ebay
Hii ni laptop ya Apple, hapo ndio imeshagawanywa nusu yani!
half-a-mailbox-der-juli-ebay1
Hili ni sanduku la barua, na lenyewe limegawanywa tayari.
half-an-iphone-5-der-juli-ebay1
iPhone nayo haikuachwa.
half-an-opel-corsa-der-juli-ebay1
Gari ndogo ya kutembelea, Opel Corsa nayo iko nusu hapo.
half-a-samsung-tv-der-juli-ebay1
TV ya Samsung nayo iko nusu.
half-a-teddy-bear-der-juli-ebay1
Mdoli nao ulikutwa na huu mkasa wa kugawanywa nusu !!
half-of-four-chairs-der-juli-ebay1
Viti vya kukalia.
Helmet
Helmet ambayo inavaliwa kichwani ukiendesha pikipiki
divorce-half-of-everything-6
enhanced-3911-1434633611-9
Hapa kuna video wakati jamaa yuko busy kabisa anagawanya vitu

Hii nusunusu unaionaje mtu wangu, iko sawa kweli? Nitafurahi kuona comment yako kwenye haya maamuzi ya mgao mtu wangu !

picha za ndani za maisha club hizi hapa na nje pia

Screen Shot 2015-06-16 at 10.20.53 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.20.37 PM

Screen Shot 2015-06-16 at 10.20.45 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.21.03 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.21.13 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.21.21 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.21.38 PM
Screen Shot 2015-06-16 at 10.21.46 PM

ona mahali maisha club ilipohamia kwa sasa ,

Screen Shot 2015-06-16 at 10.20.53 PM
ni maeneo ya makumbusho pembeni na makumbusho ya taifa yaliyopo kijitonyama .pia ni pembeni ya jengo la millenium tower ambalo watu wengi wanalijua zaidi.

ratiba ya ligi kuu uingereza hii hapa

Ratiba ya mechi za EPL yatolewa



Meneja wa Chelsea Jose Mourinho 
 
 
 
 
 
 

Chelsea itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old Trafford.

Arsenal 
 
 
null
 
 
 
 
Arsenal itaialika West Ham ,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.

Manuel Pellegrini 
 
 
 
 
 
null
 
Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita.

Tuesday, 16 June 2015

list ya wanamichezo wanaolipwa mkwanja mrefu duniani hii hapa maywether akiongoza


Floyd Mayweather Jr, mwanamichezo anayelipwa zaidi ulimwenguni
Bondia Floyd Mayweather Jr ndio mwanamichezo aliyeingiza pesa nyingi zaidi dunia katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Mayweather ameingiza kiasi cha dola milioni 300 katika kipindi cha miezi hiyo na fedha nyingi ikiwa imepatikana kutoka na pambano lake na bondia Manny Pacquiao.
Manny ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo huku nyota wa kandanda Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa wanamichezo waliotengeneza pesa nyingi.
Orodha kamili ipitie katika tovuti ya bbcswahili.com
Ifuatayo ni orodha kamili ya wanamichezo hao
1. Floyd Mayweather, US, US$300m (£194m).
2. Manny Pacquiao, Philippines, $160m (£103.4m)
3. Cristiano Ronaldo, Portugal, $79.6m (£51.4m)
4. Lionel Messi, Argentina, $73.8m (£47.7m)
5. Roger Federer, Switzerland, $67m (£43.3m)
6. LeBron James, US, $64.8m (£41.9m)
7. Kevin Durant, US, $54.1m (£35m)
8. Phil Mickelson, US$50.8m (£32.8m)
9. Tiger Woods, US, $50.6m (£32.7m)
10. Kobe Bryant, US, = $49.5m (£32m)

wakati mataifa ya afrika yanafanya vizuri katka soka eti tanzania tunaweza huu


Mcheza golf akiwajibika.
Michuano ya gofu ya Afrika (African golf Jacket) itakafanyika Windhoek, Namibia huku nchi kadhaa za Afrika ikiwemo Tanzania na Kenya zikitarajiwa kushiriki.
Nchi nyingine ni pamoja na Botswana, Afrika ya Kusini, Zimbabwe, Zambia, Msumbiji, Swaziland na wenyeji, Namibia, ambao watagharamia wageni wao
Makamu wa raisi wa chama cha gofu nchini Tanzania (TGU), Joseph Tango amesema mchezaji Abbas Adamu kutoka Arusha, Kaskazini mwa Tanzania atakuwa ni miongoni mwa washiriki, baada ya kushinda mara mbili michuano iliyopita na akiwa miongoni mwa wachezaji wa daraja la juu (Division A).
Wachezaji wengine wawili watachaguliwa kutoka division B na C na Tango atakuwa kiongozi wa msafara. “Tuna mategemeo wachezaji wetu watafanya vizuri na kurudi nyumbani na ushindi”, amesema Tango.

taarifa kamili ya raheem sterling kuondoka liverpool hii hapa.



Raheem Sterling

Liverpool imekataa ombi la kitita cha pauni milioni 25 na nyongeza ya pauni milioni 5 kutoka kwa Manchester City ili kumnunua Raheem Sterling.
Pia inaaminika kwamba Liverpool inamthamini mchezaji huyo wa miaka 20 kuwa na thamani ya pauni milioni 50 na kwamba haina mpango wa kumuuza .

mancity

Mchezaji huyo amehusishwa na mzozo katika uwanja wa Anfield na hivi majuzi alisema kuwa hatoweka sahihi ya mkataba mwengine katika klabu hiyo.
Hatahivyo ajenti wa Sterling Aidy Ward amedaiwa kusema kwamba hatokubali kandarasi nyengine katika klabu ya Liverpool hata akipewa kandarasi ya pauni laki tisa kwa wiki.

CAF kumuunga mkono INFANTINO Urais wa FIFA

Shirikisho la soka barani Afrika CAF linamuunga mkono Infantino Rais wa shirikisho la soka barani Africa (CAF) AHMAD AHMAD amesema shir...